Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yalaani mashambulizi katika vijiji magharibi mwa Niger

Watu wakitembea kwenye barabara Tillaberi eneo la magharibi mwa Niger
UNICEF/Vincent Tremeau
Watu wakitembea kwenye barabara Tillaberi eneo la magharibi mwa Niger

UN yalaani mashambulizi katika vijiji magharibi mwa Niger

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulio ya Jumamosi yaliyotekelezwa na watu waliojihami wasiojulikana katika kijiji cha Tchombangou na Zaroumbareye, eneo la Tillabéri nchini Niger.

Katibu Mkuu Antonio Guteress, ameelezea rambi rambi zake kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na watu na serikali ya Niger na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi.
Bwana Guteress kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Jumapili anatumai kwamba mamlaka Niger watafanya kila wawezalo kuwafikisha mbele ya sheria watekelezaji wa kitendo hicho cha kinyama huku wakiimarisha ulinzi wa raia.
Katibu Mkuu amesisitiza umoja na msaada wa Umoja wa Mataifa kwa serikali na watu wa Niger katika vita dhidi ya ugaidi, misimamo mikali na uhalifu wa kupangwa.