Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yatoa msaada wa dharura wa chakula kwa watoto nchini Uingereza

Aliyekuwa msakata kambumbu wa Uingereza na balozi mwema wa UNICEF David Beckham akiwa kwenye shule mjini London, UK anunga mkona kazi za shirka hilo.
© UNICEF/Dymond
Aliyekuwa msakata kambumbu wa Uingereza na balozi mwema wa UNICEF David Beckham akiwa kwenye shule mjini London, UK anunga mkona kazi za shirka hilo.

UNICEF yatoa msaada wa dharura wa chakula kwa watoto nchini Uingereza

Msaada wa Kibinadamu

Maelfu ya familia zilizoathirika na janga la corona au COVID-19 nchini Uingereza zitapokea msaada wa dharura wa chakula kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika kipindi cha sikukuu na zaidi limetangaza shirika hilo likiongeza kuwa msaada huo utakuwa ni wa mara moja tu. 

Hii ni mara ya kwanza kwa historia ya shirika hilo ambalo lina zaidi ya miaka 70, kuingilia kati na kusaidia watu wasiojiweza na walio hatarini katika taifa kile tajiri la kifalme amesema Anna Kettley mkurugenzi wa program wa UNICEF nchini Uingereza katika taarifa iliyotolewa leo.. 

UNICEF imeshirikiana na kundi linalojiita Sustain na wametoa msaada wa fedha kwa miraji 30 ya kijamii yenye lengo la kuwafikia vijana kati ya 10,000 na 15,000 mpaka program hiyo itakapomalizika mwishoni mwa mwezi Aprili 2021. Kiasi cha dola zaidi ya milioni 1 kimetengwa kwa programu hiyo. 

Msaada zaidi 

Kwa mujibu wa UNICEF msaada zaidi unajumuisha ahadi yad ola 34,000 ili kufikicha mlo wa kifungua kinywa kwa watpoto 13,5000 katika shule 25 zilizo katika eneo la Kusini mwa London katika muda wa wiki mbili za mapumziko Krisimasi na mapumziko ya nusu ya muhula wa shule mwezi Februari. 

“Msaada huu wa ufadhili utasaidia kujenga jamii imara wakati athari za COVID-19 zikizidi kubwa mbaya. Pia natoa wito wa kusaka suluhu ya muda mrefu kukabiliana na mizizi ya umasikini wa chakula ili kusiwe na mtoto yeyote anayeshinda njaa.” Ameongeza Kettley. 

UNICEF imelielezea janga la corona kama ni mgogoro mkubwa wa dharura kuwaathiri watoto tangu vita vya pili vya dunia. 

Hata kabla ya janga hili kuzuka shirika hilo linasema takriban watoto milioni 2.4 nchini Uingereza tayari walikuwa hawana uhakika wa chakula. 

Ongezeko la njaa tangu Machi 

Hali imezidi kuwa mbaya tangu mwesi Machi mwaka huu wa 2020 na familia nyingi zimekuwa zikihaha kukidhi mahitaji ya chakula na fursa za kuweza kupata chakula, huku kukiwa na mgogoro wa kiuchumi uanaoendfelea na maelfu ya watu kupoteza ajira. 

Mradi wa usaidizi wa chakula kwa kushirikiana na mdau ambaye ni School Food Matters wameanzisha mpango wa mlo wa kifungua kinywa ambao ulizinduliwa mapema mwaka huu. 

Mpango huo umerndeshwa kwa wiki 18 wakati wa amri ya watu wote kusalia majumbani  na wakati wa majira ya kiangazi ukitoa msaa muhimu na lishe kwa Watoto wenye mahitaji limesema shirika la UNICEF. “Miradi ya kijamii itakuwa na jukumu muhimu na kupitia mkakati wa nguvu ya chakula kwa kizazi cha COVID, tunatarajia kuzisaidia familia katika ngazi ya mashinani ili Watoto waendelee kula vizuri katika kipindi hiki cha mgogoro.” Ameongeza Bi. Kettley. Ambaye akijibu shutuma kwamba msaada huo wa UNICEF ni masuala ya kisiasa amesema “UNICEF inachukua hatua kukabiliana na hali hii ya mgogoro wa dharura na kwa kuzingatia uzoefu wetu wa miaka 25 ya kufanyakazi ya kuangalia haki za watoto nchini Uingereza na kutoa msaada huu wa mara moja uliozinduliwa mwezi Agosti kwa ajili ya kuzisaidia familia na watoto wasiojiweza nchini humu wakati huu wa kipindi cha mgogoro..” 

Kwa ubia na Sustain na muungano kwa ajili ya chakula na kilimo, zaidi ya paundi za Uingereza 700,000 za UNICEF zimetolewa kwa kwa makundi ya kijamii nchi zima kusaidia kazi zao za kuwasaidia watoto na familia zilizo katika hatari ya kutokuwa na uhakika wa chakula wakati huu wa janga la corona. 

“UNICEF itaendelea kutumia ufadhili wetu wa kimataifa kusaidia Watoto masikini duniani. Tunaamini kwamba kila mtoto ni muhimu na anastahili kuishi na kushamiri bila kujali wapi alikozaliwa.” Amesisitiza mkurugenzi huyo wa program wa shirika hilo nchini Uingereza.