Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mwandishi wa habari raia wa Urusi Dmitry Muratov na mshindi wa tuzo ya Nobel

Tuzo ya mshindi wa Nobel yauzwa dola milioni 103.5 fedha kugawanywa na UNICEF

UN News/Nargiz Shekinskaya
Mwandishi wa habari raia wa Urusi Dmitry Muratov na mshindi wa tuzo ya Nobel

Tuzo ya mshindi wa Nobel yauzwa dola milioni 103.5 fedha kugawanywa na UNICEF

Msaada wa Kibinadamu

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Dmitry Muratov ambaye alipiga mnada medali yake ya dhahabu ili kuchangisha fedha kwa ajili ya wakimbizi watoto Juni 20, 2022 ameiambia Idhaa ya Umoja wa Mataifa kwamba Kitendo cha medali yake kuvunja rekodi kwa kuuzwa dola milioni 103.5 kimethibitisha kwamba "wakati mwingine ubinadamu unaweza kuja pamoja, na kuoyesha mshikamano".

Mutarov ni mhariri mkuu wa kampuni huru ya habari ya nchini Urusi, Novaya Gazeta  ambayo ilifungiwa na Kremlin mwezi Machi kufuatia vikwazo vipya kwa waandishi wa habari kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Amesema yeye na wenzake walichagua fedha za tuzo hiyo kwenda kwenye Mfuko wa Umoja wa Matafa wa kuhudumua watoto katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwakuwa ni shirika bora lisilo la kiserikali kwa kazi ya kuhakikisha kuwa fedha zitawafikia watoto wote wa Ukraine wenye uhitaji.

Hiki ndicho tunachohitaji

"UNICEF haina sumu kabisa", Muratov alisema katika mahojiano maalum na Idhaa ya Urusi ya Umoja wa Mataifa kufuatia mnada huo. "Wana wataalamu bora, wana programu, wanaripoti jinsi na nini wanafanya, hii ndio tunayohitaji.

“Tuliwaandikia barua, tukapata majibu kutoka kwao, ninayo. Ilikuwa muhimu kwangu, kwamba UNICEF ilibaini kuwa pesa hizo zingeenda kwa nchi zote zinazopakana na Ukraine, ambapo wakimbizi wanapatikana - bila ubaguzi."

Amesema anatumaini watoto wa Ukraine ambao sasa walikuwa nchini Urusi, pia watafaidika: "Kuna zaidi ya wakimbizi milioni moja na nusu nchini Urusi, labda pungufu ya hapo kidogo. Kwa hiyo, tulichagua UNICEF, ambayo ina fursa kama hizo, na ambayo inaelewa vyema kwamba haina ajenda za kisiasa, bali za kibinadamu.”

Mshindi huyu wa Tuzo ya Nobel raia wa Urusi, alitunukiwa nishani ya dhahabu mwezi Oktoba 2021, pamoja na mwanahabari Maria Ressa wa Ufilipino kutokana  na kuhamasisha uhuru wa kujieleza na kuripoti bila woga licha ya unyanyasaji na vitisho vya kuuawa alisema kwamba hakuwahi katika "ndoto zake mbaya" kutarajia kwamba tuzo hiyo itaweza kupata pesa nyingi kama hizo.

Matumaini yake makubwa yalikuwa kwamba inaweza kufikia dola milioni 5 lakini kiasi walichopata kwenye mnada ni dola milioni 103.5

 Dmitry Muratov, mwandishi wa habari wa Urusi na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2021
Novaya Gazeta
Dmitry Muratov, mwandishi wa habari wa Urusi na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2021

'Uchunguzi kwa walioshiriki mnada'

Mhariri Muratov alisema kuwa kwa maombi ya UNICEF kabla ya mnada huo walifanya uchunguzi wa  kina kwa wazabuni mbalimbali, ikiwa ni pamoja na hatimaye kushinda zabuni, ili kuhakikisha kwamba chanzo cha fedha hizo si mtajiri wa Urusi au kwa jina jingine “oligarch,” au kutokana na operesheni yoyote haramu ya uhalifu kama vile binadamu au wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

"Waliangaliwa kupitia mfumo wa benki, mfumo wa kifedha, na yote ambayo ninaweza kusema kwa asilimia 100, ambayo pia niliarifiwa, kuarifiwa na kuoneshwa, ni kwamba hii ni uwazi kabisa, na fedha za uwazi", aliiambia Idhaa ya Urusi ya Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, hakutaja utambulisho wa mzabuni aliyeshinda - akioyesha kwamba hakujua jina, na kwamba kutokujulikana kumethibitiwa kuwa ni usiri: "Kama ningejua, nisingefichua, kwa sababu huu ni mgongano wa kimaslahi mtupu: watu tukakubaliana na kanuni tulizozipendekeza, halafu tutakuwa tumezichukua na kuzikiuka kanuni. Hiyo haiwezi kufanya kazi.”

Mama mmoja na mapacha wake wa umri wa miaka kumi na moja walikuwa mmoja wa wengi waliokumbwa na mkasa huo katika kituo cha treni cha Kramatorsk nchini Ukraine wakati kombora lilipopiga na kuwajeruhi mamia waliokuwa wakikimbia vita.
© UNICEF/Lviv Territorial Medical Union Hospital
Mama mmoja na mapacha wake wa umri wa miaka kumi na moja walikuwa mmoja wa wengi waliokumbwa na mkasa huo katika kituo cha treni cha Kramatorsk nchini Ukraine wakati kombora lilipopiga na kuwajeruhi mamia waliokuwa wakikimbia vita.

'Ni kosa la nchi yangu'

Akifafanua sababu nyingi kwa nini chombo chake cha habari hakikuweza kufikiria kuruhusu mzabuni wa Urusi kuingia kwenye kinyang'anyiro, au kwa nini alifikiria chombo chake kisikabidhi fedha hizo moja kwa moja kwa Serikali ya Ukraine, alisema hiyo itakuwa sio sawa kwa kuzingatia hali ya vita.

Ikiwa mwanzoni Ukraine walikuwa na hasira kidogo, sasa wamekasirika zaidi,  nchi yao inasambaratika, kutoka kwenye uso wa dunia…Unapoona haya yote kila sekunde, unakuwa na kama sauti inapiga kichwani wakati wote, unakuwa unaishi kati ya ghorofa na nyumba yakujificha kutokana mabomu…Ni kosa la nchi yangu.”