Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni vimetawala Uingereza :Achiume

Watoto wa mjini Cape Town Afrika Kusini miaka ya 1980 nyakati ambazo weusi na weupe hawakuruhusiwa kuoana.
UN
Watoto wa mjini Cape Town Afrika Kusini miaka ya 1980 nyakati ambazo weusi na weupe hawakuruhusiwa kuoana.

Ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni vimetawala Uingereza :Achiume

Haki za binadamu

Sera za serikali ya Uingereza zinachochea ubaguzi wa rangi , chuki dhidi ya wageni na kuongeza hali ya kutokuwa na usawa kwa misingi ya rangi kwa mujibu wa  ripoti ya mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa rangi na haki za binadamu.

Katika ripoti hiyo itakayowasilishwa kwenye Baraza la haki za binadamu tarehe 8 Julai E.Tendayi Achiume ametaja masuala yanayosababisha kuendelea na pengo la usawa wa kibaguzi kuwa ni pamoja na mambo mengine elimu, ajira, masuala ya nyumba, afya, watu kufuatiliwa na kamera, makabilianao na pilisi, watu kukamatwa na kuswekwa rumande.

Katika ripoti yake Bi. Achiume ameongeza kua katika masuala aliyoyoyabaini alipofanya ziara ya tathimini nchini Uingereza mwezi Aprili na Mei mwaka 2018 ni kwamba “mfumo wa kijamii na kiuchumi unawatenga jamii za waliowachache kwa misingi ya rangi na watokakona hakuna mfumo wa kisheria uliopo mahsusi kwa ajili ya kukabiliana na ubaguzi wa rangi, na ukweli unaouma ni kwamba rangi, kabila, dini,jinsia, hali ya ulemavu na vipengee vingine kama hivyo vinaendelea kuwa vigezo vya fursa za Maisha na mustakabali wa watu nchini Uingereza kwa njia mbao halikubalikina mara nyingi ni kinyume cha sheria.”

Achiume amesema alichokibaini hakiwezi kuwa ni kitu cha kushangaza kwa serikali kwani takwimu na ripota ikiwezo za ukaguzi wa pengo la kibaguzi kwa misingi ya rangi, tathimini ya Lammy na kazi ya tume ya usawa ya Uingereza vilianika wazi kuendelea kwa ubaguzi na kutenga watu kwa misingi ya rangi na jamii watokako.

Ripoti za kuaminika zimnaonyesha kwamba hatua za kukabiliana na mdororo wa kiuchumi zimekuwa na athari kubwa kwa watu wa rangi tofauti na wa jamii za walio wachache ambao ndio waathirika wa kubwa wa ukosefu wa ajarira” amesema Bi Achiume na kuongeza kwamba wakati huohuo rangi na makundi ya waio wachache ndio idadi kubwa ya watu walioko mikono ya sharia kutokana na uhalifu na wana uwakilishi Mdogo katika taasisi ambazo zinashughulikia uhalifu na adhabu.

“Kuna Ushahidi wa kutosha kwamba utekelezaji wa sharia za kupambana na itikadi kali unayalenga makundi ya watu kwa misingi ya diji na jamii watokako, kwa kukiuka haki zao za binadamu na pia imeibadilisha mifumo ya taasisi za umma kama hospitali, shule na vyuo vikuu na hata polisi , taasisi ambako kazi ya ujumuishwaji wa kitaifa ingekuwa inafanyika na kuzifanya kuwa maeneo ya kibaguzi, kutenga watu na ya kuleta hofu ya kitaifa.” Amesema Achiume

Ripoti yake imetaja pia mkakati wa uhamiaji nchini Uingereza unategemea raia binafsi na wafanyakzi wa umma kutekeleza sera za uhamiaji hali ambayo inabadili maeneo kama benki, hospitali na makazi binafsi kuwa ni vituo vya ukaguzi. Matokeo yake hali ya kitaifa dhidi ya uhamiaji ni ya ubaguzi wa rangi na kutenga watu kwa misingi ya rangi.

Akitoa mfano katika ripota yake Achiume amesema kwamba takwimu za serikali yenyewe zinathibitisha kwamba baada ya kura ya maoni ya Uingereza kutangaza kujiengua kwenye Muungano wa Ulaya (Brexit) iliambatana na ongezeko la uhalifu wa vitendo vya chuki , kupinga uhamiaji na ubaguzi wa rangi na wa misingi ya kidini.. “Kuwa bayana Brexit haijaanzisha ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni Uingereza vyote vimekuwa na miziz ya muda mrefu nchini humo tangu enzi za ukoloni na utumwa.” Amesisitiza bi Achiume.

Amekumbusha kwamba “serikali haipwasi kuchanganya ukusanyaji wa takwimu na hatua inazopaswa kuchukua kwa kuzingatia wajibu wake hini ya sharia za kimataifa za haki za binadamu. Serikali zina wajibu wa kufanya tathimini na kuchukua hatua bila kuchelewa kukomesha ubaguzi wa rangi na kuhakikisha usawa kwa watu wa rangi zote."

 

TAGS: Ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni, haki za binadamu, Uingereza, UK, E.Tendayi Achiume