Usiombe ukutwe na hali ya kukosa utaifa!  

15 Disemba 2020

Kutana na Mpho Modise, mama wa watoto wanne ambaye licha ya kuishi nchini Afrika Kusini hana uhakika wa utaifa wake na hivyo anashindwa kupata huduma za msingi kama vile afya na hofu yake kubwa ni kwamba shida inayomkabili yeye ya kukosa utaifa inaweza kuhamia kwa watoto wake labda apate utaifa wa Afrika Kusini.

Katika jimbo la Kaskazini-Magharibi nchini Afrika Kusini, tunakutana na Mpho Modise, mama wa watoto wanne ambaye hana uhakika wa umri wake kwa kuwa hana cheti cha kuzaliwa kuthibitisha hilo. Mpho hana utaifa na ana hofu kubwa. Ni kama vile nimekufa ingawa niko hai. Usiku siwezi kulala! Nafikiria kuhusu maisha yangu. Nawaza ni wapi nitaishia na hadhi yangu. Maisha yangu ni magumu. Nadhani nilitekelezwa na mtu ambaye nafikiri ni mama yangu wakati nina umri wa miaka mitano.” 

Kila aendapo aliitwa mgeni na alipigwa na Mpho hajawahi kwenda shule. Mama huyu anaamini kuwa alipokuwa na umri wa miaka 7, mtu anayedhaniwa kuwa mama yake mzazi alimtelekeza kwenye kitongoji cha Brits mwaka 1994. Tangu wakati huo amekuwa akihama kutoka makazi moja hadi mengine hadi familia zilipochoka kumchukua. 

Kwa kuwa hana nyaraka kama cheti cha kuzaliwa kuthiitisha utambulisho wake, Mpho hawezi kwenda shule. Amekuwa akisalia nyumbani akifanya kazi kama vile kuosha vyombo, kufua na kupika. Hafahamu kusoma wala kuandika. 

Mpho hafahamu hata ndugu yake mmoja ambaye anaweza kumwelezea yeye asili yake ni wapi. “Sasa nina watoto wangu mwenyewe. Kama ningalikuwa na kitambulisho, ningalifanya kazi mashambani ili kusaidia watoto wangu. Lakini nani atakuwa kazi bila kitambulisho.?” 

Hadi sasa Mpho kupitia kanisa anaendelea kusaka haki yake ya kupata utaifa na amebaini mpango wa kupeleka watoto wake waasiliwe. Hata hivyo anasema,  “Matumaini yangu ni kujiona mwenyewe kwenye nyumba yangu na watoto wangu. Nione watoto wangu wanaenda shule na wakinieleza kuwa wamemaliza masomo yao.” 

Duniani kote kuna zaidi ya watu milioni 10 wasio na utaifa na mamilioni wengine wako hatarini kupoteza utaifa wao. 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter