Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Wanawake wahamiaji na wanao kwenye kituo cha karantini Niamey, Niger.

UN yatoa ombi la dola bilioni 1 kwa ajili ya mfuko wa dharura CERF

© UNICEF/Juan Haro
Wanawake wahamiaji na wanao kwenye kituo cha karantini Niamey, Niger.

UN yatoa ombi la dola bilioni 1 kwa ajili ya mfuko wa dharura CERF

Msaada wa Kibinadamu

Umoja wa Mataifa umesema mfuko wa dharura wa Umoja huo CERF mwaka huu wa 2020 umetoa dola milioni 820 kwa ajili ya msaada wa kifedha kwa nchi 52 kote duniani.

Akizungumza mjini New york katika tukio maalum la wahisani kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko huo lililofanyika leo kwa njia ya mtandaoKatibu Mkuu Antonio Guterres amesema “Kuwekeza kwa CERF ni kuwekeza katika ubinadamu.” 

Ameongeza lengo ni kukusanya dola bilioni 1 kwa ajili ya msaada wa kifedha kwa mwaka 2021. 

Guterres amesema “CERF huwajibika haraka, haina vikwazo vya kimfumo na wakati mwingine ni chanzo pekee cha fedha kwa kukabiliana na dharura kwa sababu vyanzo vingine vinaweza kuwasili kwa kuchelewa.” 

Mama na mwana wakipokea huduma ya afya katika kituo jimboni Quneitra, Syria.
UNOCHA/Ourfali
Mama na mwana wakipokea huduma ya afya katika kituo jimboni Quneitra, Syria.

Umuhimu  

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu “CERF ni chombo kinachochagiza na kuruhusu hatua kuchukiwa katika migogoro iliyosahaulika ambayo haivutii wahisani wa kifedha.” 

Mwaka 2020 CERF imetoa dola milioni 225 kwa migogoro 20 ambayo ama ina ufadhili mdogo au iliyopuuzwa. Guterres amesema kupitia CERF mfumo wa Umoja wa Mataifa unafanyakazi Pamoja kuanzia kutathimini mahitaji hadi kupanga mipango na kutoa kipaumbele, ikiyaongoza mashirika na wadau wengine kuchukua hatua haraka na kwa kiwango kikubwa. 

Kwa Katibu Mkuu wakati wa dharura ya janga la kibinadamu CERF huleta tofauti kubwa.Mark Lowcock akizungumza katika tukio hilo amesema “Dunia hivi sasa inakabiliwa na changamoto kubwa nay a aina yake kushuhudiwa kwa vizazi kadhaa na CERF haijawahi kuhitajika kama wakati hu una hili linaweza kushuhudiwa katika sehemu zote nilizotembelea ambako unasikia hadithi za watu ambao walipata msaada kwa sababu ya CERF.” 

 

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu, Darfur, UNAMID wakifanya doria Shangil Tobaya Kaskazini mwa Darfur, Sudan.
UN Photo/Olivier Chassot
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu, Darfur, UNAMID wakifanya doria Shangil Tobaya Kaskazini mwa Darfur, Sudan.

Bwana Guterre amesema mwaka 2020 ulikabiliwa na mazingira magumu ya janga la corona au coronavirus">COVID-19 lakini “CERF imekuwa ndio muhimuli wa mafanikio. Mfuko huo umetoa dola milioni 820 kusidia nchi 52 ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi cha fedha kuwahi kutolewa katika mwaka mmoja.” 

Ameongeza kuwa msaada huo umewezesha kukabiliana na janga la nzige wa jangwani Kusini Mashariki mwa Afrika na kuwasaidia karibu watu 600,000 waliolazimika kuzikimbia nyumba zao nchini Syria baada ya mashambulizi ya anga. 

Fedha hizo pia zilitumika wakati ulipozuka mlipuko mpya wa ebola nchini DRC na kusaidia nchi nyingine kadhaa kupata vifaa vya kujingika na corona (PPE), vifaa vilivyohitajika hospitali, mnyororo wa usambazaji na kampeni za utoaji taarifa. 

Na wakati athari za janga hilo ziliposhika kasi CERF ilitenga dola milioni 220 kusaidia watu milioni 65 katika nchi 38. 

Kuzuia 

Mfuko huo wa CERF pia unasaidia miradi ya kupinga ukatili wa kijinsia na mapambano dhidi ya njaa Afrika na katika nchi za Mashariki ya Kati . 

Mwaka huu pia CERF kwa mara ya kwanza ilisaidia hatua za kuzuia majanga kwa kupeleka fedha kusaidia kukabiliana na mgogoro wa chakula Somalia na dhidi ya jaafuriko Bangladesh. 

Guterres amesema “Kusaidia watu kuchukua hatua za kukinga kuliko kuponya ni bora zaidi n ani rahisi kuliko kukabiliana na athari hapo baadaye.” 

Eneo la Tigray linakabiliwa na changamoto nyingi za kimaendeleao nchini Ethiopia. picha ya maktaba
© UNICEF/Zerihun Sewunet
Eneo la Tigray linakabiliwa na changamoto nyingi za kimaendeleao nchini Ethiopia. picha ya maktaba

Ufadhili 

Mwaka 2016 Baraza Kuu liliidhinisha wito wa Katibu Mkuu wa kuongeza ufadhili wa mwaka kwa CERF na lengo ni kufikia dola bilioni 1. Na mwaka 2019 nchi wanachama na wadau wengine walichangia dola milioni 835 lakini mwaka huu wa 2020 fedha zilizochangwa hadi sasa n idola milioni 495. 

Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu amesema “Dola bilioni 1 ni kiwango cha chini cha kuweza kuwasaidia watu waliokwama katika dharura mbalimbali.” 

Amewaomba wahisani kutoa ahadi kwa zaidi yam waka akisema kwamba “Hakikisho na uhakika wa fedha unaruhusu CERF kutekeleza majukumu yake kikamilifu. Na uwekezaji kwa CERF ni uwekezaji katika ubinadamu.”