Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 172 wafa na zaidi ya 500 washukiwa kuambukizwa homa ya manjano Nigeria:WHO

Dozi moja ya chanjo dhidi ya homa ya manjano humpatia mtu kinga ya maisha dhidi ya ugonjwa huo hatari
WHO
Dozi moja ya chanjo dhidi ya homa ya manjano humpatia mtu kinga ya maisha dhidi ya ugonjwa huo hatari

Watu 172 wafa na zaidi ya 500 washukiwa kuambukizwa homa ya manjano Nigeria:WHO

Afya

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limesema mlipuko mpya wa homa ya manjano nchini Nigeria umeshakatili maisha ya watu 172 na wengi 530 wanashukiwa kuambukizwa homa hiyo. 

Akizungumza na waandishi wa Habari kwa njia ya mtandao mjini Geneva Uswis hii leo msemaji wa WHO Tarik Jasarevic amesema tangu mwaka 2017 Nigeria imekuwa na mafaniko katika mapambano dhidi ya milipuko ya homa ya manjano lakini mlipuko mpya uliobainika mapema mwezi Novemba mwaka huu umesababisha vifo vingi katika majimbo yote matano ya nchi hiyo. 

Shirika hilo linasema nchi hiyo ambayo imekuwa ikikabiliwa na milipuko mingine ya magonjwa ya kuambukiza kama corona auu coronavirus">COVID-19 na mgogoro wa kibinadamu kwa sababu ya machafuko Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo imepata changamoto kubwa ya kudhibiti masuala yote kwa wakati mmoja. 

Bwana Jasarevic amesema “Mbali ya vifo hivyo 1732 katika visa 530 vinavyoshukiwa visa 48 vimethibitishwa maabara na mapambano dhidi ya homa hiyo yanakabiliwa na mtihani kwa sababu hivi sasa Nigeria inakabiliwa pia na homa ya Lassa, usambazaji wa chanjo ya polio, surua, ugonjwa unaofanana na tetekuanga ambao ulisababishwa na nyani waliokuwa wakifanyiwa utafiti uuitwao monkeypox na kipindupindu, pamoja na mgogotro wa kibinadamu uliosababishwa na vita Kasskazini Mashariki mwa taifa hilo la Afrika Magharibi.” 

WHO imekuwa ikiisaidia wizara ya afya ya Nigeria kukabiliana na mlipuko wa sasa, kuzuia mlipuko huo kusambaa katika nchi jirani zilizo katika hatari kubwa kwa kutoa chanjo muhimu ya kuzuia ugonjwa huo. 

Tangu mwaka 2004 kampeni ya chanjo ya homa ya manjano imekuwa ikiendeshwa mara kwa mara nchini Nigeria ili kuongeza kiwango cha kuwalinda watu. 

Hivi sasa WHO imependekeza chanjo dhidi ya homa ya manjano kwa wasafiri wote wa kimataifa wanaoingia Nigeria kuanzia watoto wa umri wa miezi 9. Pia shirika hilo limesisitiza kwamba chanjo inayotolewa dhidi ya homa ya manjano ni muhimu, inafanyakazi vizuri, ni ya gharama nafuu na inatoa ulinzi wa maisha dhidi ya homa hiyo kwa wanaoipata.