Mikakati ya kupambana na homa ya manjano, Uganda

31 Januari 2020

Uganda, imeimarisha juhudi za kudhibiti mlipuko wa homa ya manjano kaskazini magharini na magharibi ya kati mwa nchi wakati huu ambapo tayari watu wanne wameaga dunia kutokana na mpuko wa homa ya njano kama anavyosimulia mwandishi wetu John Kibego katika ripoti ifuatayo.

Wizara ya afya ya Uganda katika ushirikiano na shirika la afya ulimwenguni (WHO), ilithibitisha na kutangaza mlipuko wa virusi vya homa ya manjano hapo tarehe 27 januari katika wilaya za Moyo kaskazini magharibi mwa Uganda na Buliisa magharibi ya kati mwa nchi.

Inasema kwa sasa kuna visa vinne vya mambukizo ikiwemo watatu waliofariki dunia. Mwanaume mmoja alikufa kufa katika wilaya ya Buliisa na wengine wawili katika wilaya ya Moyo.

Waliofariki dunia walikuwa ni  wafanyabaishara ya kuvuka mipaka kwenda Sudan Kusini na Jamhuri ya Kiddemokrasia ya Congo (DRC).

Kwa mantiki hiyo mamlaka za mitaani kwa msaada kutoka kwa wadau wake ikiwemo WHO, zimeimarisha juhudi za kudhibiti virusi hivyo visisambae humo nchini na katika nchi jirani hasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC na Sudani kusini.

Afisa wa afya wa wilaya ya Buliisa Dkt.Neslson Naisye ameniambia kuwa, “kati ya sampuli 7 zilizopimwa, mmoja amegunduliwa na virusi hivyo tukiwa tunazungumuzia kipindi cha miezi miwili kutoka Novemba. Bila shaka tunaendelea na ufuatiliaji kubaini kiwango cha mlipuko na sababu zake. Kwa sasa tumebaini kuwa wathirika wote ni wafugaji”

Serikali ya Uganda imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuitikia uwezeshaji wa kutoa chanjo dhidi ya virusi vya homa hiyo hatari huku ikiwa na mipango ya kujumwisha chanjo dhidi ya homa ya manjano katika chajo za kawaida.

Mwenyekiti wa wilaya ya Buliisa Simon Agaba Kinene amesema wamaimarisha usalama mpakani na juhudi za kuhamasisha jamii na pia tayari wameafikiana kutumia hema iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya ebola itumike kushughulikia kwa kwa kiasi fulani wilaya hiyo imejikinga dhidi ya ebola, “Tutatoa msaada wowote unaotakiwa kujiandaa kama vile tumekuwa tukifanya kuzuia ebola kuingia. Tutatumia hema ile iliyokuwa kwa ajili ya ebola kushughulikia hali ya mlipuko huu kwa sasa”

Kuhara, kutapika, homa, maimivu ya kichwa, ngozi kugeuka rangi ya njano na kukojoa damu ni miongoni mwa dadili za homa ya manjano.

Mipango ya kudhibiti gonjwa hili inaendelea wakati ambapo tishio lililo kubwa zaidi la virusi vya corona vinavyosambaa kutoka China vinasambaa kwa kasi duniani.

Hiki ni kigezo kikubwa kwa nchi za Afrika mashariki kwani huenda ikakumbwa na changamoto ya uhaba wa rasilimali za kupambana na majanga manne makubwa. Mosi ni la homa ya manjano, pili ni tishio la muda mrefu la ebola kutoka DRC, tatu ni virusi vya corona kutoka China na pia uvamizi wa nzige unaoyubisha uhakika wa chakula nchini Kenya.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter