Homa ya manjano

Muuguzi akiandaa chanjo ya kuchanja mtoto katika kliniki Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
© UNICEF/Thomas Nybo

Mikakati ya kupambana na homa ya manjano, Uganda

Uganda, imeimarisha juhudi za kudhibiti mlipuko wa homa ya manjano kaskazini magharini na magharibi ya kati mwa nchi wakati huu ambapo tayari watu wanne wameaga dunia kutokana na mpuko wa homa ya njano kama anavyosimulia mwandishi wetu John Kibego katika ripoti ifuatayo.

Sauti
2'44"

WHO yasaidiana na serikali ya Congo-Brazaville kudhibiti homa ya manjano

Nchini Jamhuri ya Congo, serikali kwa kushirikiana na shirika la afya duniani, WHO na wadau wengine wameendesha kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano kwenye mji wa bandari wa Pointe Noire na maeneo ya jirani.  Grace Kaneiya na ripoti kamili.

Katika moja ya kliniki mjini Pointe Noire, jamhuri ya Congo, watu wamepanga foleni kupata chanjo dhidi ya homa ya manjano.

Sauti
2'4"

Watu milioni 25 kuchanjwa dhidi ya homa ya manjano Nigeria:WHO

Shirika la Aflya ulimwenguni WHO kwa ushirikiano na serikali ya Nigeria, wamezindua kampeni kabambe  na kubwa kuwahi kufanyika ya chanjo dhidi ya  homa ya manjano kwa mwaka wa 2018 ikiwa na lengo la kuwafikia watu wapato milioni 25 kazikazini mwa Nigeria.

Kampeni hiyo iliozinduliwa  rasmi hii  leo ni  moja ya kampeni za kimataifa kusuhu chanjo ya homa ya manjano  kwa udhamini na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF  pamoja na  GAVI unaolenga haswa majimbo ya kazikazini mwa Nigeria ya kogi, kwara na Zamfara, na baadae Borno.

Chanjo milioni 1.4 za homa ya manjano kuokoa maisha Nigeria:WHO

Kundi la kimataifa la kuratibu utoaji wa chanjo ya homa ya manjano (ICG) limetoa dozi  milioni 1.4 za chanjo ya homa ya manjano kwa ajili ya kampeni itakayoanza kesho Jumamosi Desemba pili ili kusaidia kudhibiti mlipuko wa homa ya manajano unaoendelea nchini Nigeria.

Serikali ya Nigeria kwa msaada wa shirika la afya ulimwenguni WHO na wadau wengine inatarajiwa kuwachanja watu milioni 1.3 katika kudhibiti mlipuko huo kwenye maeneo yaliyoathirika.