Virusi visivyojulikana vipatavyo 850,000 viko kwa wanyama na ndege na vinaweza kuathiri binadamu :IPBES/CBD Ripoti

29 Oktoba 2020

Ripoti mpya iliyotolewa leo na jukwaa la kimataifa la sera za kisayansi kuhusu bayoanuai na huduma za mifumo ya viumbe (IPBES) na kutathiminiwa na mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya bayoanuai (CBD), imeonya kwamba majanga makubwa ya milipuko ya magonjwa yako njiani laki hatua madhubuti zikichukuliwa hatari inaweza kupunguzwa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kuna virusi 540,000 hadi 850,000 visivyojulikana kwenye mazingira yetu ambavyo bado vinaweza kuambukizwa kwa watu, na inatabiriwa kwamba siku za usoni milipuko ya mgonjwa ambayo ni majanga makubwa  yanaweza kutokea mara kwa mara, yatasambaa haraka, yatasababisha gharama na athari kubwa za kiuchumi na kuua watu wengi zaidi ya janga la sasa la corona au COVID-19 endapo hakutofanyika mabadiliko makubwa katika mtazamo wa kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza. 

Je ripoti hii iliyopewa jina “Bayoanuai na milipuko ya majanga ya magonjwa” ambayo imeandaliwa na wataalam 22 kutoka kote duniani inamaanisha nini? Dkt. Elizabeth Mrema katibu mtendani wa CBD anafafanua 

(SAUTI YA ELIZABETH MREMA CUT 1) 

Pia ameeleza uhusiano uliopo baina ya maliasili, mazingira na milipuko ya magonjwa ya kuambukiza. 

(SAUTI YA ELIZABETH MREMA CUT 2) 

Na nini kifanyike sasa kuepusha hatari ya majanga hayo kama COVID-19 siku zijazo?  Dkt. Mrema anasema

(SAUTI YA ELIZABETH MREMA CUT 3) 

Ripoti hiyo imesema COVID-19 ni janga la sita la kimataifa la kiafya tangu kutokea kwa mlipuko mkubwa kabisa wa mafua duniani wa mwaka 1918 na kwa kiasi kikubwa limechochewa na shughuli za binadamu. 

Ripoti inakadiria kwamba virusi vingine milioni 1.7 ambavyo bado havijabainiwa vipo miongoni mwa wafanyama na ndege na 850,000 kati ya virusi hivyo vinauwezo wa kuambukizwa kwa binadamu. 

TAGS: IPBES, CBD, COVID-19, virusi, Dkt. Elizabeth Mrema

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter