Shirika la afya ulimwenguni WHO jana Alhamisi limetangaza kuwa virusi vipya vya corona ni dharura ya afya ya kimataifa inayotia wasiwasi likizitaka nchi zote kuchukua tahadhari na kujiandaa endapo virusi hivyo vitazuka katika nchi zao. Kwa sasa virusi hivyo kitovu chake kimekuwa mji wa Wuhan nchini China ambako Kwa mujibu wa WHO jumla ya visa 9692 vimethibitishwa katika majimbo 31, na kati ya hivyo watu 1239 wako katika hali mbaya, 213 wamefariki dunia na wagonjwa 103 wametibiwa, kupona na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Na nje ya China kuna visa 68 vilivyothibitishwa katika nchi 18.