Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya changamoto ushirikiano Maziwa Makuu waendelea kuimarika: Xia

Muuguzi aliyepona corona au COVID-19 amerejea kazini kuwasaidia wagonjwa wengine katika hospitali nchini Rwanda
© UNICEF
Muuguzi aliyepona corona au COVID-19 amerejea kazini kuwasaidia wagonjwa wengine katika hospitali nchini Rwanda

Licha ya changamoto ushirikiano Maziwa Makuu waendelea kuimarika: Xia

Amani na Usalama

Ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika licha ya kupambana na changamoto ya janga la corona au COVID-19 umeendelea kuimarisha ushirikiano wa kisiasa, kiusalama na kiuchumi kwa kuzingatia makubaliano yam waka 2013, amesema mjumbe maalum wa umoja wa Mataifa kwa ajili ya ukanda huo Huang Xia.

Akitoa taarifa kwenye Baraza la Usalama hii leo kwa njia ya video kutokea Nairobi Kenya, kuhusu hali ya ukanda huo Xia amesema“Licha ya changamoto zilizopo na sasa janga la COVID-19 watu wa Ukanda wa Maziwa Makuu wameendelea kuonyesha mnepo mkubwa na dhamira ya kusonga mbele”.

Bwana. Xia ambaye mara ya mwisho alitoa taarifa kwenye Baraza la Usalama mwezi Aprili mwaka huu amesema katika miezi michache iliyopita hali katika ukanda huo wa maziwa Makuu imesalia kuwa tulivu na yenye hatua za kutia matumaini.

Kutatua tofauti kwa njia ya kidiplomasia

Mjumbe huyo maalum wa Umoja wa Mataifa ametaja hatua za kisiasa za hibvi karibuni kama vile kukabidhiana madaraka kwa njia ya amani nchini Burundi kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Mei, na mkutano mdogo uliofanyika mapema mwezi huu kuhusu ushirikiano wa mssuala ya usalama na uchumi uliojumuisha viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Angola, Uganda na Rwanda.

“Pia nakaribisha ukweli kwamba nchi katika ukanda huu zinatumia njia za kidiplomasia na mikakati ya kikanda kutatua tofauti zao kama ilivyodhihirika katika kutatua mzozo wa mpaka baina ya DRC na Zambia.”Amesema Bwana. Xia na kuongeza kuwaNia ya Rwanda na Uganda kuendeleza mchakato wa kurejesha katika hali ya kawaida uhusiano wao kupitia usuluhishi wa Angola na DRC ni mfano mwingine chanya.”

Xia Huang, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Ukanda wa Maziwa Makuu
UN News/ Cristina Silveiro
Xia Huang, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Ukanda wa Maziwa Makuu

Madhila yasiyovumilika kwa raia DRC

Hata hivyo Xia ameelezea hofu yake kuhusu hali tete ya mchafuko yanayoendelea Mashariki mwa DRC ambako makundi yenye silaha yanaendelea kuwa sababu ya madhila yasiyovumilika kwa raia. Ametoa wito kwa Baraza la Usalama kuongeza hatua.“Ukwepaji sheria unaofurahiwa na watekelezaji wa uhalifu unawaumiza rai ana kuathiri vibaya uhusiano baina ya nchi za uakanda wa Maziwa Makuu. Hivyo ni lazima tuimarishe juhudi zetu kupambana na ukwepaji sheria.”

Bwa. Xia pia ameainisha mipango ya kusaidia utekelezaji mkakati wa ushirikiano wa amani, usalama na uchumi uliotiwa saini 2013, kwa lengo la kushughulikia miziz ya vita na mzunguko wa machafuko Mashariki mwa DRC na Ukanda mzima wa Maziwa Makuu.

Kuunga mkono amani, usalama na ushirikiano

Kazi ya mjumbe huyo maalum imejikita katika vipaumbele vitano ikiwemo kuchagiza msaada wa kimataifa baada ya kuzuka janga la corona au COVID-19.

Na msaada ambao umekusanywa kwa ajili ya nchi hizo au Ukanda huo hadi sasa ni mkubwa lakini bado hautoshi kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha duniani IMF.

“Ili kuzindua upya ombi hilo natoa wito kwa wadau wa kimataifa kuwezesha mchango wa kifedha kwa nchi hizi ikiwemo mradi wa kuwapunguzia au kufuta madeni.”

Xia pia amezungumzia juhudi zake zingine za kidiplomasia ambazo zinajumuisha kuchagiza mazungumzo nah atua ambazo si za kijeshi katika masuala ya usalama, kama vile mipango ya upokonyaji silaha, kuwaondoa askari vitani na kuwajumuisha katika jamii wapiganaji wa zamani.

Mwaka huu ni maazimizo ya miaka 20 ya azimio la kihistora la Baraza la Usalama namba 13 25 kuhusu wanawake, amani na usama na mjumbe huyo ambasema baadhi ya nchi za Maziwa Makuu ni miongoni mwa nchi zenye uwakilishi mkubwa wa wanawake hasa bungeni ingawa bado kuna changamoto.

Mkakati wa amani wa Umoja wa Mataifa

Mjumbe huyo pia amelieleza Baraza la Usalama kuhusu mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kuleta amani, kuzuia migogoro na kutatua mizozo katika Ukanda wa Maziwa Makuu ambao umeandaliwa na ofisi yake.

Amesema nchi hizo na washirika wa kikanda wamechangia katika kuandaa nyaraka ambazo zimewasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Mkakati huo umeweka hatua zitakazochukuliwa na Umoja wa Mataifa katika ukanda huo kwa muongo mmoja ujao, ukijikita katika nguzo kuu tatu : amani, usalama na haki, maendeleo endelevu na kushirikiana mafanikio, na mnepo dhidi ya changamoto za zamani na mpya.

Na hatua hizo amesema zitalenga hususan maeneo ya diplomasia, usalama, ushirikiano, maendeleo, kuchagiza haki za binadamu na kuimarisha jukumu la wanawake na vijana.