Chuja:

Maziwa Makuu

Watu Asili kushiriki na kushirikishwa katika utunzaji wa mazingira na viumbe hai: Burundi

Kongamano la watu asili kutoka  eneo la Maziwa makuu  barani Afrika limehitimishwa mjini  Bujumbura Burundi . Lilijikita katika jinsi Jamii hiyo wanavyoweza kushiriki na  kushirikishwa katika utunzaji wa mazingira na viumbe hai katika maeneo wanakoishi.

Jamii hiyo imekuwa inanyooshewa kidole kwa kuhusika na sehemu kubwa katika uharibifu wa mazingira, madai ambayo wanayakana wakitaja kwamba mazingira ni sehemu ya maisha yao.

Kutoka bujumbura , Muandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA amefuatilia kongamano hilo na kuandaa makala hii.

Sauti
4'4"

Wanawake wanolewa huko DRC

Harakati za kujumuisha wanawake katika usuluhishi na utatuzi wa migogoro huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo, DRC zinashika kasi baada ya wanawake kushiriki kwenye warsha ya kuwapatia stadi hizo. Ikiandaliwana mkutano wa kimataifa wa Maziwa Makuu, ICGLR, warsha hiyo imefanyika katika zama za sasa zilizogubikwa na mvutano wa kisiasa kutokana na vuta ni kuvute kuhusu uchaguzi mkuu nchini humo na baadhi ya watu wakitaka Rais Joseph Kabila ajiuzulu kuelekea uchaguzi. Mwakilishi kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO Taib Diallo amesema wanawake wamepatiwa stadi za kushiriki