Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upatanishi ni dawa mujarabu ya kutokomeza mizozo:Guterres

Katibu Mkuu wa UN  António Guterres (kwenye mimbari) akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 6 wa upatanisho , Istanbul Mediation Conference nchini Uturuki  31 Octoba 2019.
UN Photo/Emrah Gruel
Katibu Mkuu wa UN António Guterres (kwenye mimbari) akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 6 wa upatanisho , Istanbul Mediation Conference nchini Uturuki 31 Octoba 2019.

Upatanishi ni dawa mujarabu ya kutokomeza mizozo:Guterres

Amani na Usalama

Upatanisho ni dawa mujarabu ya kumaliza migogoro na mkutano huu wa 6 wa Istanbul kuhusu upatanishi ni fursa muhimu ya kufikiria ni jinsi gani tunaweza kuchukua mtazamo wa suala hili ambalo ni moja ya nyezo muhimu za kupunguza na kutokomeza kabisa migogoro.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mastaifa Antonio Guterres mjini Istanbul Uturuki kunakofanyika mkutano huo. Guterres amesema wakati mgogoro wa Syria ukiendelea kwa mwaka wa 8 sasa huku raia wakilipa gharama kubwa ya maisha yao katika vita hivyo kulikuwa hakuna mwelekeo thabiti wa suluhu ya kisiasa lakini “Mkutano wa kwanza wa kamati ya katiba ya Syria uliofanyika mjini Geneva Uswis ulikuwa wa kihistoria na msingi wa hatua zinazopigwa na htua hiyo ni hali dhahiri wa mafanikio ya upatanisho. Natumai hii itakuwa hatua ya kwanza kuelekea suluhu ya kisiasa ambayo itamaliza ukurasa huu wa madhila na machungu kwa watu wa Syria na pia kuunda fursa kwa wote kuweza kurejea katika maeneo yao ya asili kwa usalama na ut una kumaliza hali waliyonayo ya ukimbizi.”

Takriban wWasyria milioni 13.1 wanahitaji msaada , milioni 6.6 ni wakimbizi wa ndani , takriban milioni 1 wengine ama wako katika maeneo yanayozingirwa au yasiyofikika, na wakati huohuo zaidi ya Wasyria milioni 5.6 wamefungasha virago na kuikimbia nchi yao tangu mwaka 2011 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Wakati akikaribisha majadiliano ili kukomesha mzozo wa Kaskazini Mashariki mwa Syria Guterres ameuambia mkutano mjini Istanbul bado ana hofu kuhusu hali ya Idlib kwa upande wa Magharibi, na amerejea wito wake kwamba kila pande husika katika mzozo inapaswa kujizuia , kuacha machafuko na kuwalinda raia na miundombinu yao katika kila kona. Amepongeza pia matokeo mazuri ya upatanishi hususan katika nchi za Afrika na kumtaka kila mmoja kuendeleza juhudi za mafanikio haya.

Benki ya Teknolojia ya Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alipotembelea Benki ya Teknolojia ya Umoja wa Mataifa akiwa na Mustafa Varank, Waziri wa viwanda na Teknolojia wa Uturuki mjini Gebze, Uturuki (31 Oktoba 2019)
UN Photo/Emrah Gruel
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alipotembelea Benki ya Teknolojia ya Umoja wa Mataifa akiwa na Mustafa Varank, Waziri wa viwanda na Teknolojia wa Uturuki mjini Gebze, Uturuki (31 Oktoba 2019)

 

Baadaye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea Makao Makuu ya Benki ya teknolojia  kwa ajili ya nchi zinazoendelea na kuiita benki hiyo kuwa ni ishara chanya na hatua ya moja kwa moja kuelekea ahadi ya ajenda ya mwaka 2030 ya kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.

Ili kuondoa pengo linalofahamika kama mgawanyiko wa kidijitali kwa watu bilioni mbili ambao bado hawajaunganishwa katika intaneti, benki ilifunguliwa kaatika jiji la Gebze mwaka jaana. Benki hiyo inafadhiliwa kwa kutegemea michango ya hiari.

Bwana Guterres amesisitiza kwamba wakati inapoanzisha ubia ndani na nje ya mfumo wa Umoja wa Mataifa, Benki hiyo ilikuwa ikiboresha uratibu wa uvumbuzi wa sayansi na teknolojia katika nchi zilizoendelea na itachukua jukumu muhimu katika Ushirikiano wa Kusini, na kwa ulimwengu wote unaoendelea.