UN yataka uchunguzi huru kuhusu kupewa sumu kiongozi wa upinzani Urusi Alexei Navalny

8 Septemba 2020

Katika taarifa yale iliyotolewa mjini Geneva Uswisi Bi. Bachelet amesema "Alexei Navalny, jana Jumatatu ameamka kutoka kwenye koma katika hospitali ya Charité mjini Berlin ambako alipelekwa baada ya kudhuriwa na sumu mnamo Agosti 20 kwenye mji wa Siberia nchini Urusi."

Kamishina huyo ameitaka serikali ya Urusi kufanya uchunguzi wa kina au kutoa ushirikiano katika uchunguzi wa wazi, huru na usio na upendeleo.

Akikaribisha taarifa za kiongozi huyo wa upinzani kutoka kwenye koma Bi. Bachelet amekumbusha kwamba wataalam wa kitabibu wa Ujerumani wamesema wana ushahidi kwamba alipewa sumu.

Ameongeza kuwa tarehe pili Septemba Berlin Ujerumani ambako kulifanyika uchunguzi wa kitabibu katika maabara ya kijeshi  kuhusu hali ya kiongozi huyo wa upinzani ilitangazwa kwamba "kuna ushahidi usiopingika kuwa kiongozi huyo wa upinzani alikuwa ni muhanga wa kupewa sumu inayoathiri mishipa ya fahamu au Novichik-type nerve agent."

"Kasamishina mkuu amesema sumu hiyo inayoathiri mishipa na sumu zingine za mionzi kama Novichok na polonium-2010 ni dawa za hali ya juu na ni vigumu sana kuzipata, hivyo ameongeza "hili linazusha maswali mengi, kwa nini kutumia dawa za sumu kama hizi? nani anazitumi? walizipataje? Ni uhalifu mkubwa sana uliotekelezwa kwenye ardhi ya Urusi" amesisitiza Bachelet.

Mkuu huyo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa anaamini kwamba, "kukataa kufanyika kwa uchunguzi wa kina, huru, usio na upendeleo na wa wazi kuhusiana na jaribio hilo la mauaji hakutokidhi majibu yanayohitajika. Ni wajibu wa serikali ya Urusi iliyoko madarakani kuchunguza kwa kina waliohusika na uhalifu huo. Ni uhalifu mkubwa sana uliotendeka katika ardhi ya Urusi."

Kamishina Mkuu huyo ameongeza kuwa "idadi ya visa vya kupewa sumu au mifumo mingine ya mayaji ya kulengwa kwa Rais wa Urusi au raia wa zamani wa nchi hiyo au kwingineko katika miongo miwili iliyopita inatia hofu kubwa. Na hatua ya kushindwa kuwawajibisha wahusika katika visa vingi au kuhakikisha haki inatendeka kwa waathirika au familia zao ni suala la kusikitisha sana na ni vigumu kulielezea au kulihallisha."

Nani anayehusika na uhalifu huo

Alipoulizwa kuhusu waliohusika na uhalifu huo , msemaji wa ofisi ya haki za binadamu mjini Geneva Rupert Colville , amelaani kitendo hicho cha kumzuru kiuongozi wa upinzani kwa sumu.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao Coville amesema "siko katika nafasi ya kumshutumu yeyote kuhusu hili."

Tarehe 20 Agosti Alexeï Navalny alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahtuti kwenye hosputali ya Omsk, Siberia,baada ya kuugua akiwa ndani ya ndege iliyokuwa ikisafiri kutoka katika mji wa Tomsk kuelekea mji mkuu wa Urusi,  Moscow.

Kiongozi huyo wa upinzani wa Urusi ambaye aliingia kwenye koma alisafirishwa agosti 22 hahi hospitali mjini Berlin Ujerumani kwa ombi la familia yake .

Madaktari wa Ujerumani katika hospitali ya Charité walisema tarehe 24 kwamba kiongozi huyo alionyesha dalili za kupewa sumu.

Bwana Colville ameongeza kuwa kwa upande wa ofisi ya haki za binadamu tunakumbuka kwamba hata kabla ya Alexei Navalny kupewa sumu alikuwa akibughudhiwa, kukamatwa na kufanyiwa ukatili mara kadhaa, ama na mamlaka au watu wasiojulikana, "Navalny alikuwa ni mtu ambaye kwa hakika alihitaji ulinzi kutoka kwa serikali ingawa likuwa ni kiongozi wa upinzani katika masuala ya kisiasa." amesema Bi. Bachelet.

 

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter