Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtoto 1 kati ya 2 duniani anapitia ukatili na nchi zimeshindwa kuuzuia:UN

Msichana wa miaka mitano akicheza katika nyumba ya familia yao huko Kazakhstan, ambapo UNICEF inafanya kazi kumaliza ukatili wa majumbani kupitia matembezi ya nyumbani
© UNICEF/Anush Babajanyan
Msichana wa miaka mitano akicheza katika nyumba ya familia yao huko Kazakhstan, ambapo UNICEF inafanya kazi kumaliza ukatili wa majumbani kupitia matembezi ya nyumbani

Mtoto 1 kati ya 2 duniani anapitia ukatili na nchi zimeshindwa kuuzuia:UN

Amani na Usalama

Ripoti mpya iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kimataifa ya kuzuia ukatili dhidi ya watoto imeonya kwamba nchi zimeshindwa kuzuia ukatili huo dhidi ya watoto na kutoa wito kwa nchi kuchukua hatua kuzuia athari kubwa zaidi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo nusu ya watoto wote duniani sawa na takribani  watoto bilioni moja kila mwaka wanaathirika na ukatili wa kimwili, kingono au kisaikolojia, kujeruhiwa, kusababishiwa ulemavu na kifo kwa sababu nchi zimeshindwa kuzingatia mikakati iliyowekwa ya kuwalinda watoto.

Ripoti hiyo iliyotolewa kwa Pamoja na shirika la afya duniani WHO, la kuhudumia Watoto UNICEF, la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili dhidi ya watoto na End Violence Partnership.

Ushahidi kuhusu ukatili huo

Akizungumzia kuhusu ukatili huo mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhaanom Ghebreyesus amesema “Hakuna udhuru wowote kwa ukatili dhidi ya Watoto. Tuna ushahidi wa nyenzo za kuzuia ukatili huo ambapo tunazitaka nchi zote kutekeleza. Kulinda afya na ustawi wa Watoto ni kiini cha kulinda afya yetu ya Pamoja na ustawi sasa na siku za usoni.”

Ripoti hiyo iliyopewa jina “Ripoti ya hali ya kimataifa katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto 2020” ni ripoti ya kwanza ya aina yake ikiainisha hatua zilizopigwa katika nchi 115 chini ya mkakati wa INSPIRE ambao unajumuisha mikakati saba kwa ajili ya kuzuia na kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto.

Ripoti imebainisha bayana haja ya nchi zote kuongeza juhudi kutekeleza mikakati hiyo. Wakati karibu nchi zote (88%) zina sharia muhimu za kuwalinda Watoto dhidi ya uktili , chini ya nusu ya nchi hizo (47%) zimesema mikakati hiyo inatekelezwa ipasavyo.

Ripoti hiyo kwa mara ya kwanza imejumuisha makadirio ya mauaji ya watoto hususan walio chini ya umri wa miaka 18. Makadirio ya siku za nyuma yalitokana na takwimu ambazo zilijumuisha vijana wa miaka 18 hadi 19 na imebaini kwamba mwaka 2017 karibu Watoto 40,000 walikuwa wahanga wa mauaji.

Ukatili umesababisha zaidi ya watoto milioni 1.9 kusitisha masomo magharibi na Afrika ya Kati
UNICEF/Jiro Ose
Ukatili umesababisha zaidi ya watoto milioni 1.9 kusitisha masomo magharibi na Afrika ya Kati

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Henrietta Fore amesema “Ukatili dhidi ya watoto siku zote umekuwa ni changamoto na sasa hali itakuwa mbaya zaidi. Hatua za watu kusalia majumbani, shule kufungwa na vikwazo vya kutembea vimewaacha Watoto wengi wakiwa wamekwama na watu wanaowatendea ukatili, bila kuwa na maeneo salama ambayo shule hutoa mara nyingi. Ni muhimu kufanya kazi haraka kuchukua hatua kuwalinda watoto wakati huu wa na zaidi ikiwemo kuwa na huduma maalum ya wafanyakazi wa ustawi wa jamii na kuimarisha msaada kwa watoto.

Hatua zilizopigwa hazilingani

Kupitia mikakati ya INSPIRE fursa za shule tu kupitia Watoto kusajiliwa ndio zilizoonyesha hatua kubwa huku asilimia 54 ya nchi zikiripoti kwamba idadi kubwa ya Watoto wenye mahitaji walifikiwa kwa njia hiyo.

Nch zsilimia 32 hadi 37 zinachukulia mwamba waathirika wa ukatili wanaweza kupata msaada, wakati asilimia 26 ya nchi zimetoa msaada kwa wazazi na walezi.

Pia ripoti inasema asilimia 21ya nchi zina mipango ya kubadilisha mila mbaya na asilimia 15 ya nchi zimefanya mabadiliko ili kutoa mazingira salama kwa ajili ya watoto.

Ingawa asilimia 83 ya nchi zina takwimu za kitaifa kuhusu ukatili dhidi ya Watoto ni asilimia 21 pekee ya nch ilitumia takwimu hizo kuwea msingi na malengo ya kitaifa kuzuia na kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto.

Kwa mujibu wa ripoti asilimia 80 yya nchi zina mipango ya kitaifa na sera lakini ni moja ya tano tu ya nchi hizo ndiozo zilizo na mipango ambayo imefadhiliwa kikamilifu  zina malengo yanayopimika.

Ukosefu wa fedha za ufadhili na uwezo wa wahudumu waliohitimu ni miongoni mwa sababu zinachochangia kwa nini utekelezaji umekuwa chini.