Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa UNICEF wa mafunzo kwa waendesha boda boda ni nuru kwa wanawake wajawazito Uganda

Usafiri wa pikipiki uitwao bodaboda maarufu kama 'mshikaki'
Benki ya Dunia/Stephan Gladieu
Usafiri wa pikipiki uitwao bodaboda maarufu kama 'mshikaki'

Mradi wa UNICEF wa mafunzo kwa waendesha boda boda ni nuru kwa wanawake wajawazito Uganda

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa kushirikiana na taasisi ya Sweden kwa ajili ya maendeleo ya kimataifa imeanzisha mfumo wa usafiri wa boda boda kwa ajili ya kusafirisha wanawake na watoto hadi kwenye vituo vya afya.

Katika wilaya ya Zombo, Nile magharibi, kaskazini mwa Uganda kuptia mradi huo wa UNICEF waendesha boda boda 133 wamepokea mafunzo maalum kwa ajili ya kusimamia ufikishaji wa wanawake wajawazito walio na dalili za kujifungua na watoto wagonjwa kuweza kufika kwenye kituo cha afya.

Otim Tony ni msimamizi katika kituo cha afya cha Alangi

(Sauti ya Otim)

“Walipokea mafunzo pia ya kuwawezesha kuhudhumia wanawake wajawazito iwapo inafika muda wa kujifungua kabla ya kuwasili kwenye kituo cha afya.”

Edson Mungurieki ni mwendesha boda boda kwenye jamii hiyo

(Sauti ya Edson)

“Mara ya mwisho ilitokea ilikuwa ni mwezi Mei, nilipigiwa simu saa nane alfajiri, mama alikuwa karibu anajifungua, kwa hiyo niliamua kusubiri mtoto na nikamsadia baada ya hapo nikampeleka mama na mtoto kwenye kituo cha afya.”

Kwa upande wake mama Anne Fuarega ameshuhudia faida za uwepo wa boda boda hizo

(Sauti ya Anne)

“Kwa upande wa ugonjwa, kuna wakati ambapo mtoto wangu wa tatu aliugua na mwendesha boda boda alikuja na kunipeleka sehemu ambako mtoto alitibiwa vizuri. Huo ndio uzuri wa boda boda.”

Tangu ulipoanza mradi huo, idadi ya wanawake ambao wanafika katika kituo cha afya imeongezeka kutoka akina mama 30 hadi sabini kwa mwezi.

Mradi umewezesha pia ukarabati wa wadi ya kujifungua na kuimarishwa kwa kituo cha afya cha Alangi kwa ajili ya wanawake wajawazito.