Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miradi ya UNHCR na EU yaleta nuru kwa wakimbizi na wenyeji makazi ya Kolobeyei, Kenya

Wachuuzi wakiuza bidhaa zao sokoni
Photo: FAO/Carl de Souza
Wachuuzi wakiuza bidhaa zao sokoni

Miradi ya UNHCR na EU yaleta nuru kwa wakimbizi na wenyeji makazi ya Kolobeyei, Kenya

Wahamiaji na Wakimbizi

Soko la mboga mboga la Natukobenyo linaloendeshwa na wakimbizi na jamii zinazowahifadhi ni moja ya miradi inayofadhiliwa na muungano wa Ulaya magharibi mwa Kenya katika makazi ya Kalobeyei kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Katika soko hili tunakutana na Celestine Eto mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ni mchuuzi katika soko hili jipya na wakimbizi na wenyeji wanatumia miundombinu ya kisasa ikiwemo chumba cha baridi cha kuhifadhia mboga mboga kinachotumia mkaa na maji kuhakikisha bidhaa zinasalia na ubora wake. Bi Celestine anasema anafurahia soko hili jipya na kwamba

(Sauti ya Celestine)

Hivi karibuni kamishna wa muungano wa Ulaya kwa ajili ya ushirikiano wa kimataifa Jutta Urpilainen ametembelea makazi ya Kalobeyei kwa ajili ya kukutana na wakimbizi na Wakenya walionufaika na mradi huu .

(Sauti ya Jutta)

“Miundombinu hii ambayo inatumika kwa ajili ya maisha na kutoa matumani kwa watu inatia moyo sana, natumai kwamba tunaweza kujifunza kutokana na maarifa haya amabayo yanatolewa hapa kama sehemu ya mkakati kwa Afrika.”

Mnufaika mwingine wa mradi wa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi Kolobeyei ni John Lokulu, mkimbizi kutoka Sudan Kusini ambaye yeye na familia yake ya watu sita walikimbilia Kenya mkwa 2016 na aliwekwa kwenye makazi ya muda na UNHCR lakini kwa sasa ameweza kujenga nyumba ya kudumu kutumia programu ya shirika hilo ya kutoa pesa taslimu ya CBI, “nyumba yangu inapendeza. Niliwaza muundo wake na nikatafuta fundi uashi kutoka katika jamii ya hifadhi ya Turkana ili kuijenga. UNHCR ilitupatia mafunzo kuhusu jinsi ya kusimamia mchakato wa ujenzi na tuliweza kujadili na wauzaji kupata bei nafuu kwa bidhaa za ujenzi na kuokoa fedha.”