Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa makazi ya kudumu wa UNHCR ni faida kwa wakimbizi na wenyeji Kakuma- Kenya

 wakimbizi wakiwa katika kambi ya Kakuma ,Kenya.
UNHCR/R. Gangale
wakimbizi wakiwa katika kambi ya Kakuma ,Kenya.

Mradi wa makazi ya kudumu wa UNHCR ni faida kwa wakimbizi na wenyeji Kakuma- Kenya

Wahamiaji na Wakimbizi

Katika kuondokana na njia zilizozoeleka za utoaji misaada kwa wakimbizi kambini, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Kenya linatumia mpango wa kuwapatia wakimbizi fedha taslimu ili waweze kutangamana na wenyeji wao, mfano ukiwa ni mradi wa kuwapatia fedha ili waweze kujenga makazi yao.

Video ya UNHCR inaonyesha taswira ya makazi ya kuhifadhi wakimbizi ya Kolobeyei kwenye kambi ya kakuma nchini kenya.Ujenzi wa nyumba unaendelea kupitia mpango ulionzishwa na shirika hio mwaka jana wa 2018.

Tangu kuanza kwa mradi huo  UNHCR kuwa inawapatia wakimbizi fedha taslimu kupitia benki kwa ajili ya kujenga makazi ya kudumu ili kuhakikisha makazi salama na yenye kujali utu huku wakipunguza utegemezi wa misaada na kuimarisha ujumuishwaji wa wakimbizi kupata huduma za benki na kushughulikia suala la ulinzi. 

Moffat Kamau ni msimamizi wa mradi wa pesa taslimu UNHCR

(Sauti ya Kamau)

“Wakimbizi wataweza kununua vifaa vya ujenzi kutoka kwa wafanya biashara na wengi wa wauzaji ni jamii wanaowahifadhi na mafundi ni kutoka kwa wakimbizi lakini pia jamii inayowahifadhi.”

Mmoja wa wanufaika wa mradi ni Florence Idiongo mwenye umri wa miaka 25 kutoka Sudani Kusini ambaye alikimbia mwaka 2016 na kwa kipindi cha miaka miwili yeye na familia yake waliishi katika mahema ya plastiki kwenye makazi ya Kolobeyei. 

Anasema hali ikuwa ngumu sana lakini kufuatia mradi huo wa UNHCR aliweza kujenga nyumba mbili za kudumu kwa ajili ya familia yake ya watu 12.

(Sauti ya Florence)

“Unaweza kununua nguo kwa ajili ya watoto na unaweza kununua godoro, viti na mapazia hapa ndani na utahisi salama kwa sasa watu wana utulivu.”

Mradi pia unazingatia gharama kwani wakimbizi wanajenga nyumba za kudumu kwa gharama ya chini ya asilimia 11-14 ikilinganishwa na gharama ya wadau. 

Wakimbizi wanamiliki mchakato wa ujenzi na wanashirikiana na jirani zao kujenga makazi yenye vyumba kuanzia 12 hadi 14 kwa wastani wa siku 22. 

Hii inawawezesha kutumia fedha zinazosalia kwa ajili ya mahitaji mengine na kuchangia katika uchumi wa jamii zinazowahifadhi na hivyo kuimarisha mahusiano.