Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa majiko ya mkaa unaokoa watu pamoja na msitu wa Virunga

Majiko sanifu ni muarobaini siyo tu kwa mazingira bali pia kwa afya ya wanawake ambao mara nyingi huhusika na masuala ya upishi.
Benki ya Dunia/Peter/Kapuscinski
Majiko sanifu ni muarobaini siyo tu kwa mazingira bali pia kwa afya ya wanawake ambao mara nyingi huhusika na masuala ya upishi.

Mradi wa majiko ya mkaa unaokoa watu pamoja na msitu wa Virunga

Ukuaji wa Kiuchumi

Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo unatekeleza mradi wa kuwasaidia waathirika wa ukatili wa kijinsia na kingono (SEA). Mamia kwa maelfu ya wanawake nchini DRC hivi sasa wanafaidika na miradi mbalimbali iliyoanzishwa na Mpango wa Umoja wa Mataifa, MONUSCO.

Mmoja wa miradi kati ya miradi mingi mingine, ni wa kutengeneza majiko ya mkaa ambayo si tu yanawasaidia wanawake kujipatia kipato, bali pia pamoja na faida nyingine, unasaidia kutunza mazingira hususani msitu wa Virunga ulikuwa hatarini kutokana na ukataji miti. Katika makala hii Anold Kayanda anafafanua zaidi maelezo ya Aksanti Katebera Moses, anayewafundisha wanawake utengenezaji wa majiko hayo ya mkaa maarufu kwa jina mbabulaa.