Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunasisitiza uchunguzi huru na wa haki kwa mauaji ya Khashoggi:UN

Stéphane Dujarric, Msemaji wa Umoja wa Mataifa
Picha ya UN/Jean-Marc Ferré
Stéphane Dujarric, Msemaji wa Umoja wa Mataifa

Tunasisitiza uchunguzi huru na wa haki kwa mauaji ya Khashoggi:UN

Masuala ya UM

Umoja wa Mataifa leo umeendelea kusisitiza kwamba kuhusu mauaji ya mwandishi wa Habari wa Saudia Jamal Khashoggi kinachotakiwa ni uchunguzi huru, usio na upendeleo ili kuhakikisha kuhakikisha uchunguzi kamili, na uwajibikaji, kwa ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa katika kesi hiyo.

Akijibu swali  mwandishi wa Habari hii leo mjini New York Marekani aliyetaka kujua Umoja wa Mataifa unasemaje? Kuhusu hukumu iliyotangazwa leo na mwendesha mashitaka wa saudia , msemaji wa Umoja huo Stephane Dujarric amesema "Tunazingatia ripoti za leo kwamba watu wanane amekutwa na hatua na kuhukumiwa na mahakama ya jinai ya Riyadh kuhusu mauaji ya Jamal Khashoggi. Katibu Mkuu pia anaendelea kusisitiza ahadi  ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha uhuru wa kujieleza na ulinzi wa waandishi wa habari, na pia upinzani wetu wa muda mrefu kuhusu adhabu ya kifo. "

Kwa mujibu wa duru za Habari mwendesha mashtaka wa umma wa Saudi Arabia leo Jumatatu amesema watu 5 wamehukumiwa kifo na wengine watatu kufungwa jumla ya kifungo cha miaka 24 kwa sababu ya mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Jamal Khashoggi yaliyofanyika huko Istanbul Uturuki mnamo Oktoba mwaka jana.

Lakini maafisa wakuu wawili walioshtakiwa katika kesi hiyo walifutiwa mashitaka kwa sababu ya "kutokuwepo na Ushahidi wa kutosha,"amesema  mwendesha mashtaka.

Pia naibu mwendesha mashitaka mkuu Shalaan Al-Shalaan ameuambia mkutano na waandishi wa Habari kwamba “Tumegundua kwamba mauaji ya Khashoggi hayakuamuliwa," Mahakama ya Riyadh ilifanya vikao tisakusikiliza kesi ya Khashoggi na uamuzi umetolewa leo katika kikao cha kumi.

TAGS: Khashoggi, haki za binadamu, Saudi Arabia, kesi, UN