Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake huuzwa kama bidhaa Afghanistan

Mwanamuziki na mwanaharakati wa haki za wasichana na wanawake Afghanistan, Sonita Alzadeh. Picha: World Bank/Video capture

Wanawake huuzwa kama bidhaa Afghanistan

Licha ya jumuiya ya kimataifa kupaza sauti dhidi ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, hali ni tofauti nchini Afghanistan ambapo inaelezwa kuwa wasichana huuzwa kama bidhaa, wakilazimishwa kufungishwa ndoa.

Hili limemsukuma mwanamuziki na mwanaharakati Sonita Alzadeh kutumia muziki kufikisha ujumbe wa ukomeshaji wa vitendo hivi vinavyokiuka haki za binadamu, kwani ni sawa na usafirishaji haramu wa binadamu.

Ungana na Joseph Msami katika makala iliyosheheni burudani ya muziki wa kufokafoka ikofokea vitendo hivyo.