Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR leo imezindua mkakati wa kimataifa wa nishati endelevu 

Mkaa unaotokana na miti unachangia katika uharibifu wa mazingira lakini sasa ukwajukwaju watumika huko Ethiopia kuandaa mkaa
FAO/Giulio Napolitano
Mkaa unaotokana na miti unachangia katika uharibifu wa mazingira lakini sasa ukwajukwaju watumika huko Ethiopia kuandaa mkaa

UNHCR leo imezindua mkakati wa kimataifa wa nishati endelevu 

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kwa kutambua ongezeko la changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kuinua uwezo wa wakimbizi katika kupata fursa za nishati salama na endelevu, huku likipunguza athari katka ka mazingira, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limezindua mkakati wa kimataifa wa miaka minne kwa ajili ya nishati endelevu. 

Mkakati huo unachagiza kuhamia kwenye nishati safi, mbadala na endelevu kwenye makambi ya wakimbizi na vutuovya uhifadhi ikiwemo katika nyumba binafsi, maeneo ya jamii na vituo vya msaada. 

“Hakuna njia ya kuwepa ukweli kwamba mabadiliko ya tabianchi yanachangia sababu za vita na watu kutawanywa. Kuanzia ukame na njaa hadi majanga yatokanayo na hali ya hewa ,athari za mabadilikoya tabianchi zimekuwa zikishuhudia mara kwa mara sasa sehemu mbalimbali duniani kwa wasio jiweza  na waliotengwa, ikiwemo wakimbizi na jamii zinazowahifadhi” amesema mkurugenzi wa programu ya usaidizi na mipango ya UNHCR Andrew Harper. 

Kwa mujibu wa makadirio ya sasa ya UNHCR zaidi ya asilimia 90 ya wakimbizi katika makambi wana fursa ndogo ya kupata nishati ya umeme,na hivyo kufanya kuwa vigumu kwao kupika, kufanya nyumba zao kuwa na joto linalohitajika,kusoma, kufanya kazi au kupata njia nyingine mbadala wakati wa usiku na hivyo kuwaweka katika hatari nyingi za kiafaya na kiulinzi. 
Kutokuwa na nishati mbadala 

Ukosefu wa nishati salama shirika hilo la wakimbizi limesema kumesababisha wakimbizi wengi kutumia kuni au mkaa kukidhi mahitaji yao muhimu ya nyumbani wakati jamii na vituo mbalimbali vya msaada vikitumia mafutaya dizeli kuendesha jenereta. Na vyanzo vyote hivi vya nishati vina gharama kubwa kwa mazingira na kifedha. 

“Wengi wa watu waliotawanya au kufurushwa husakahifadhi katika maeneo yasiyojiwezaduniani” amesema Harper na kuongeza kuwa “hali hii inaleta changamoto kubwa ana za kibinadamu na kimazingira. Tunahitaji kuhakikisha kwamba wale waliolazimika kukimbia wanaweza kukidhi mahitaji yao ya msingi ya nishati wakiwaukimbizi na wakati huohuo wakipunguza uharibifu wa mazingira na kulinda maisha ya jamii zinaowahifadhi.” 

UNHCR imekuwa ikifanya kazi kwa miongo kadhaa sasa kujaribu kupunguza athari za kimazingira zitokanazo na mgogoro wa wakimbizi ikiwemo kuanzisha miradi mbalimbali ya sola mfano kwenye kambi ya wakimbizi ya Za’atari nchini Jordan, kutoa nishati safi ya kupikia Niger,nishati safi na kusafisha taka kwa ajili ya wakimbizi Bangladesh, na nishati mbadala na safi ya kupikia kwa ajili ya wakimbizi nchini Rwanda, Tanzania na Ethiopia. 

Malengo ya mkakati mpya 

Mkakati huo mpya umejikita katika masula makuu manne: Kuhakikisha kwamba wakimbizi wanakidhi mahitaji yao ya nishati tangu mwanzo wa dharura, kuboresha fursa ya wakimbizi kupata nishati safi, salama ya gharama nafuu na endelevu ya kupikia na kupasha joto na kutoa mwanga kwenye nyumba zao na mwisho kuhakikishaupatikanaji wa nishati safi ya kuendesha jamii ya wakimbizi na vituo vya usaidizi kamavile mtambo mkuu wa kusambaza maji, taa za barabarani, shule na vituo vya afya. 

Ili kutekeleza mkakati huu UNHCR itachagiza na kuwezesha fursa za upatikanaji wa nishati safi kwa wakimbizi na jamii za watu waliotawanywa huku ikishirikianakwakaribu na makampuni ya utoaji nishati kuchagiza kuunganishwa na gridi ya taifa pamoja na mifumo ya nishati mbadala kuweza kuwasaidia wote wakimbizi na jamii zinazowahifadhi