Masafa ya Redio ni muhimu kwa utabiri wa hali ya hewa, yalindwe:WMO

24 Oktoba 2019

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO, limetoa wito kwa serikali kulinda masafa ya redio yaliyowekwa kwa ajili ya huduma za uangalizi duniani ambayo ni muhimu sana kwa utabiri wa hali ya hewa na ufuatiliaji wa muda mrefu wa mabadiliko ya tabianchi.

WMO imesema kutafanyika maamuzi makubwa ambayo yatakuwa na athari kwa udadisi wa masuala ya dunia, ufuatiliaji wa mazingira na operesheni za setilaiti za utabiri yatakayofanwa kwenye mkutano wa dunia wa mawasiliano ya redio utakaofanyika kuanzia tarehe 28 Oktoka hadi tarehe 22 Novemba mwaka huu.

Mkutano huu hufanyika kila baada ya miaka mitatu au minne chini ya usimamizi wa muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU na hufanya tathimini ya sheria za redio ambazo zinasimamia matumizi ya masafa na mitambo ya setilaiti na utafikiria udhibiti wa upunguzi wa nji za mawasiliano na masafa kwa ujumla.

Kumekuwa na wasiwasi unaoongezeka katika jamii ya utabiri wa hali ya hewa kwamba kuna ongezeko la ushindani wa kugombea bandwithi ikiwemo kwenye huduma za simu data za kisasa , 5G labda kutokana na kuanzisha apu zinazohusiana na setilaiti za uangalizi wa masuala ya dunia, ndege, mitambo ya radio,rada, na mifumo mingineya ufuatiliaji.

Mwenyekiti wa kundi la uratibu wa masafaya Redio la WMO Eric Allaix anasema “WMO bila shaka haitaki kuwa kikwazo katika utoaji wa teknolojia mpya za mawasiliano kama 5G. Lakini tunahofiakwamba wasiingilemasafa yanayotumika na mitambo ya kuokoa maisha kama vile ya kutabiri hali ya hewa.”

Ameongeza kuwa kuna haja ya kuwepo kwa uwiano baina ya biashara ya mda mfupi na matakwa ya teknolojia , na maisha na usalama wa muda mrefu.”Tusichukue hatari za kubadili mafanikio makubwa tuliyofikia ya kutoa tahadhari ya huduma kwa ajili ya majanga ya asili na uwezekano wa kuongeza hasara ya kupoteza maisha na mali.”

WMO inasema kwa kupitia hatua za mapema za utabiri wa hali ya hewa nakutoa tahadhari maisha mengi ya watu yameokolewa katika miongo ya karibuni na hatua hizi moja kwa moja zimachangiwa na matumizi ya masafa ya redio yaliyoko mashambani ambayo hutuma moja kwa moja utabiri kutumia mifumo iliyowekwa na kupawa watu taarifa za uhakika zaidi na muda mrefu wa kujiandaa.

Lakini WMO imeonya kwamba kuna ongezeko la shinikizo hivi sasa kutumia masafa ya redio kutoka kwenye teknolojia ya mitandao isiyohitaji nyaya na apu zingine ikiwemo huduma za mawassiliano ya kimataifa ya mitambo ya simu za rununu (IMT) ambayo inajumuisha teknolojia mpya kama 5G.

WMO na ITU wameshirikiana na kufanyakazi pamoja kwa miaka mingi kulinda masafa haya ya redio kupitia sharia za ITU zihusuzo masafa ya redio, lakini mashirika hayo yanasema hivi sasa suala hili liko mikononi mwa nchi wanachama wa mashirika haya kuzingatia utafiti wa kisayansi na kuhakikisha kwamba ulinzi unaotakiwa unapatikana na ni endelevu.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter