Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yaaani vikali shambulio la leo uwanja wa ndege Somalia

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, James Swan akihutubia Baraza la Usalama.
UN Photo/Manuel Elías
Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, James Swan akihutubia Baraza la Usalama.

UN yaaani vikali shambulio la leo uwanja wa ndege Somalia

Amani na Usalama

Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulio lililofanyika leo Jumapili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aden Adde nchini Somalia.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema shambulio hilo halikubaliki na limeathiri pia maskani ya mpango wa Umoja wa afrika nchini Somalia AMISOM na sehemu ya eneo la Umoja wa Mataifa. 

Guterres amewatakia nafuu ya haraka majeruhi wote katika shambulio hilo. Duru za habari zinasema shambulio hilo limejeryhi takriban watu sita wanaokaa kwenye makazi ya AMISOM na Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu amerejelea kauali yake kwamba anawaunga mkono wafanyakazi wote wa Umoja wa Mataifa Somalia na kwamba Umoja wa Mataifa umejizatiti kuendelea kuisaidia serikali ya Somalia na Wasomali wote katika azma yao ya kusaka amani na utulivu.

Ujumbe wa UNSOM

Naye mwakili wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ambaye pia ni mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSOM bwana James Swan, amelaani vikali shambulio hilo la mjini Moghadishu ambapo roundiza risasi zilimiminika katikamakazi ya AMISOM na Umoja wa Mataifa na kujeruhi watu kadhaa.

”Nimeshikitishwa na kuchukizwa na kitendo hili cha kigaidi dhidi ya watu wetu ambao wanafanyakazi na watu wa Somalia katika masuala ya kibinadamu, ujenzi wa amani na maendeleo. Tunashukuru kwamba wafanyakazi wetu wengi hawajaathirika, nawatakia wafanyakazi wenzu waliojeruhiwa nafuu ya haraka. Hakuna sababu yoyote inayohalalisha vitendo vyovyote vya kikatili na Umoja wa Mataifa umedhmiria kuendelea kuisaidia Somalia katika mchakato wa kusaka amani, utulivu na maendeleo.”

Hadi sasa hakuna shirika au kikundi chocote kilichodai kuhusikana shambulio hilo.