Mauaji yaliyotekelezwa kwenye hekalu yanaashiria chuki dhidi ya wayahudi-Guterres

9 Oktoba 2019

Mauaji ya watu wawili nje ya hekalu nchini Ujerumani leo Jumatano yametajwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Antonio Guterres kama “tukio la kuashiria chuki dhidi ya waayahudi.”

Shambulio hilo kwenye mji wa Halle, mashariki mwa Ujerumani yalitokea katika siku kuu ya wayahudi ya Yom Kippur, ambayo ni siku takatifu kabisa kwenye mwaka wa wayahudi.

Bwan  Guterres kupitia taarifa ya msemaji wake iliyotolewa jijini New York, Mareknai amelaani vikali shambulizi hilo ambapo amesema matukio kama hayo yanahitaji kupingwa kwa nguzu zote.

Duru zinasema kwamba mtekelezaji wa shambulio hilo alikuwa amevali mavazi yanayofanana na sare za kijeshi na alikuwa na kamera ya kunasa video ambayo alikuwa akitumia kuonyesha mbashara mashambulizi hayo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud