Iraq mnapaswa kuruhusu waandamanaji kutoa madukuduku yao:UN

4 Oktoba 2019

Misururu ya maandamano imekuwa ikishuhudiwa kote nchini Iraq wiki hii, kupinga uhaba wa ajira na kutokuwepo usawa katika utoaji wa huduma za msingi imesema ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa wengi wa waandamanaji ni vijana wasio na ajira wanaotaka haki zao za kiuchumi na kijamii ziheshimiwe.

Taarifa iliyotolewa na Marta Hurtado kutoka ofisi hiyo ya haki za binadamu amesema

Tunazikumbusha mamlaka za Iraq kuwa hayo ni matakwa muhimu, na kuwa matakwa hayo yanastahili kusikilizwa. Mamlaka zina wajibu wa kutumia kila namna kuwassaidia raia wake kujikimu ikiwemo kushughulikia suala la ukosefu wa ajira. Mamlaka nazo zinastahili kuruhusu watu wake kuelezea matakwa yao kwa njia ya amani, alisema msemaji wa kamishna wa shirika la haki za binadamua la Umoja wa Mataifa,

Ameongeza kuwa wanawasiwasi kufutia ripoti kuwa vikosi vya usalama vinatumua risasi  za moto na zile za plastiki katika baadhi ya sehemu. Na kwamba wamerusha mabomu ya kutoa machozi kwenye wimbi la waandamanaji.

Ofisi ya haki za binadamu la Umoja wa Mataifa imethibitisha vifo vya watu 12 mjini Baghdad. Hata hivyo Hurtado amesema kuwa kuna ripti ambazo hazijathibitishwa kuwa hadi watu 30 wameuawa kwenye maandamano katika miji kadhaa nchini Iraq. Mamia ya watu wameripotiwa kujeruhiwa wakiwemo wa vikosi vya ulinzi. Waandamanaji kadhaa wamekamatwa licha kuwa wengine waliachiliwa. Amesisitiza kuwa

“Tunatoa wito kwa serikali ya Iraq  kuruhusu watu kutekeleza haki yao kujieleza na kukusanyika kwa amani. Matumizi  yoyote ya nguvu yanastahili kuwepo kuambatana na viwango vya haki za binadamua vya kimataifa.”

Amesema kuna wasi wasi kuhusu ripoti iliyotolewa ikisema kuwa takriban waandishi Habari watatu waliokuwa wakifuatilia maandaano hayo wamekamatwa na wawili kati yao kuachiliwa. Pia amesema kuna ripoti za kuziliwa kwa huduma na mitandao ya kijamii katika sehemu tofauti za nchi hiyo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud