Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kituo cha ustawi wa jamii Lebanon chaleta nuru kwa mtoto mwenye mkimbizi mwenye usonji

Baadhi ya mashirika ya UN kama vile UNICEF na UNHCR yameunda vifaa na kuja na mbinu kwa maafisa wa afya kuweza kutambua mapema usonji katika jamii.
UNICEF
Baadhi ya mashirika ya UN kama vile UNICEF na UNHCR yameunda vifaa na kuja na mbinu kwa maafisa wa afya kuweza kutambua mapema usonji katika jamii.

Kituo cha ustawi wa jamii Lebanon chaleta nuru kwa mtoto mwenye mkimbizi mwenye usonji

Afya

Ingawa Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia chepuo watu wenye matatizo ya usonji wasitengwe wala kuenguliwa kwenye harakati za maendeleo yao, nchini Iraq, hali ni tofauti kwa mtoto Samer mwenye umri wa miaka 10 ambaye ameishi na upweke hadi kituo kimoja nchini Lebanon kilipoleta nuru kwenye maisha yake

 

Ni mtoto Samer katika moja ya vituo vya ustawi wa jamii nchini Lebanon. Maisha ya Mosul nchini Iraq yalikuwa ya upweke. Hapa Lebanon angalau anatumia muda mrefu kuwepo dirishani kwani ndio mlango wake wa dunia nyingine. Catrina Youssef ni mama mzazi wa Samer..

’ Huwa anawangalia wapita njia, huyapungia mkono magari yanayopita hapa na kuwatizama watoto wengine wakicheza. Huwa anawapigia kelele na kucheka.Hiyo ndiyo njiya yake ya kucheza nao.”

Samer alipofikisha umri wa   miaka miwili ikagundulika kuwa  ana tatizo la usonji,  hali ambayo inamzuia mgonjwa kushindwa kuwasiliana na jamii na pia kutokuwa na mbinu za kuzungumza.

Samer alihitaji shule maalum na usimamizi bora  na ilikuwa vigumu huko Mosul Iraq kutokana na vita vya muda mrefu na familia yake haikuweza kumudu gharama za kumpeleka maeneo mengine ya Iraq.

Baada ya vita kushamiri Mosul walikimbilia hapa Lebanon ambako Samer alipata bahati ya kuandikishwa kwenye kituo cha ustawi wa jamii ambako kwa mara ya kwanza anajifunza jinsi ya kuishi na kuwasiliana pamoja na kucheza na watoto wengine.

Na huyu ni Jessica Frem  mfanyakazi katika kituo hicho kinachomilikiwa na shirika la kiraia, Caritas.

‘’Wakati familia ilipotueleza kuhusu changamoto yake kubwa ambayo  ilikuwa kuhimili mazingira yake, tuliwaeleza kile ambacho tunafanya kwenye kituo hiki.”

Kwa kuwa Samer ndiye mtoto pekee mwenye usonji katika kituo hiki, awali mambo yalikuwa magumu lakini baadaye alizoea

Jessica ambaye ni mfanyakazi wa kituo hiki anaeleza..

“ Polepole nao watoto wakamzoea Samer na jinsi walivyomzoea sasa ni kama familia moja na hivyo ni mafafiki.”

Nchini Lebanon kuna watoto wakimbizi kutoka Iraq takriban 111 wanaohitaji matunzo maalum na 13 kati yao wana matatizo ya usonji.