Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Angelina Jolie azuru Mosul, kuwajulia hali waathirika wa vita

Mjumbe maalum wa UNHCR Angelina Jolie akiwa na kijana kutoka Iraq, Chikook, Baghdad
UNHCR
Mjumbe maalum wa UNHCR Angelina Jolie akiwa na kijana kutoka Iraq, Chikook, Baghdad

Angelina Jolie azuru Mosul, kuwajulia hali waathirika wa vita

Wahamiaji na Wakimbizi

Mjumbe maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Angelina Jolie ametembelea magharibi mwa mji wa Mosul, nchini Iraq ambalo mwaka jana lilikombolewa  kutoka kwa wanamgambo wa ISIL.

Ziara yake hiyo inakuja wakati Umoja wa Mataifa na wadau wake wanajiandaa kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 20 mwezi Juni.

Wakati wa ziara hiyo kwenye mji huo wa kale, alishuhudia majengo yaliyoathiriwa na wakati wa vita vya kuukomboa.

Katika ujumbe wake Bi Jolie ameweka bayana umuhimu wa ujenzi upya wa makazi ya raia  walioathirika na vita na pia uwezeshwaji wa wakimbizi na mahitaji mbalimbali ya kibinadamu wakati wanajaribu kurudi katika hali yao ya  zamani.

"Maisha yao yamewekwa rehani kwasababu ya vita kila wakati. Hawezi kurudi nyuma, au kusonga mbele, na kila mwaka wana chini???? (sielewi hapa una maana gani) ya kuishi."

Na kuhusu nini kifanyike kuepuka migogoro inayoendelea na kuwaathiri mamilioni ya familia nyingi duniani kote, Bi Jolie amesema.

"Jibu pekee ni kukomesha migogoro ambayo inawalazimu watu kukimbia nyumba zao. Halikadhalika serikali zote zizingatie wajibuwao wa kuwalinda raia."

Hii ni mara ya tano kwa Bi. Jolie ambaye ni mcheza filamu mashuhuri wa Marekani kutembelea Iraki katika ziara 61 tangu kuteuliwa kwake  kama mjumbe maalum wa UNHCR.

UNHCR inasaidia familia nyingi zinazorudi nyumbani ikiwa ni pamoja na usaidizi wa fedha ili kujenga nyumba zao, usaidizi wa kisheria kwa familia ambazo zimekuwa vizuizini kwa sababu ya utambulisho usio sahihi, na kusaidia kupata hati muhimu za kisheria ambazo zilichukuliwa, kuharibiwa au kukataliwa wakati walikuwa chini ya utawala wa ISIL.