Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya tunasonga ingawa bado tuko mbali-Kenyatta

Rais wa Uhuru Kenyatta wa Kenya wakati akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
UN Photo/Cia Pak
Rais wa Uhuru Kenyatta wa Kenya wakati akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Kenya tunasonga ingawa bado tuko mbali-Kenyatta

Masuala ya UM

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema nchi yake inajitahidi katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu na imepiga hatua ingawa bado kuna safari ndefu.

Akihutubia mjadala Mkuu wa mkutano wa 74 wa  Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA74,  unaoendelea kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New Yorl amesema kila nchi inajukumu la kujitokeza katika jukumu la pamoja ili kuhakikisha kizazi hiki na kijacho kinasalimika. Na kwamba “kaulimbiua ya mkutano wa mwaka huu ya kuchagiza juhudi za ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya kutokomeza umasikini , elimu bora , hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na ujumuishwaji imekuja katika wakati muafaka kwani inatusaidia kujihusisha na masuala mbali mbali tata na changamoto za kimataifa zinazoikabili dunia leo hii”.

Ameongeza kuwa kwa pamoja “Tunawajibu wa kuhakikisha dunia ni mahala bora pa kuishi kwa ajili ya kizazi kijacho, lazima tuhakikishe tunawaanda watoto wetu katika mazingira ya utulivu wa kisiasa mazingira bora na kuishi pamoja kwa ushirikiano katika duniani hii. Na sisi viongozi tuliokusanyika hapa leo ni lazima tuwe daraja la azima hiyo.”

Rais Kenyatta amesema hatua zinazochukuliwa leo hii na dunia ndizo zitatanabahi mustakabali wa kizazo kijacho kama utakuwa bora , au ulioshiwa rasilimali , ukiwa na kiwango cha juu cha umasikini au na hali ya hatari ya mgawanyiko mkubwa katika dunia.Na endapo hatua muafaka zitachukuliwa basi mustakbali wa kizazi kijacho utakuwa wa mafanikio, uliosheheni rasilimali na mshikamano wa kimataifa.

Pia Rais huyo wa Kenya ametaja mambo matatu ambayo yataweza kuchangia mustakabali bora ambao dunia inautamani, “Mosi ni lazima kuwawekawatu kuwa kitovu cha maendeleo  , ni lazima kuwasaidia watu wetu na kuwashirikisha hususan vijana ili kujenga mustakabali na sio kuwa waathirika wa mustakbali huo na kutomuacha yeyeote nyuma.

Na kwa upande wa Kenya amesema wamefanikiwa kutoa elimu bure kwas hule za msingi na za kutwa za upili, pi inapambana na maradhi na iko mbioni kutimiza elengo la Hhuduma za afya kwa wote ifikapo 2022. Na ili kuhakikisha wasicha wanapata fursa sawa ya elimu Rais Uhuru amesema wameanzisha upya mkakati wa kuwarejesha shuleni wasichana walioacha shule kwa ajili ya kupata ujauzito, na sasa wanatoa taulo za kike bure kwa wasichana wote wanaohudhuria shule. Wameongeza idadi ya wananchi wanaopata huduza za afya na bima ya afya.

Pili amesema huwezi kuwa na mendeleo endelevu bila amani akitolea mfano changamoto inayoendelea Pembe ya Afrika  na tatu amesema ni lazima kuchukua hatua kwa pamoja ili kulinda mustakbali wa dunia hii.

Amehitimisha kwa kusema mwezi Novemba mwaka huu serikali ya Kenya kwa ushirikiano na shirika la idadi ya watu duniani UNFPA wataiisha mkutano wa kimataifa wa idadi ya watu na maendeleo ambao utatoa mwangaza na malengo ya kuyatekeleza katika kufanikisha SDGs