Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikutano 5 ya kuifuatilia wakati wa UNGA74

Ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifajijini New York Marekani
UN/Eskinder Debebe
Ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifajijini New York Marekani

Mikutano 5 ya kuifuatilia wakati wa UNGA74

Masuala ya UM

Ni mwaka mwingine na wakati mwingine na fursa nyingine ambapo macho na masikio ya dunia yanaelekezwa jijini New york kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa , wakati viongozi wa dunia wakiwasili kushiriki kwenye mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa au UNGA.

Mwaka huu mjadala wa UNGA 74 mbali ya hotuba za kawaida kutoka kwa wakuu w anchi na serikali mikutano mitano ya ngazi ya juu  itafanyika ikiangazia masuala muhimu yanayoikabili dunia hivi sasa

Mitano.

Tuvalu ambalo ni taifa la kisiwa kwenye bahari ya Pasifiki liko ukanda wa chini na hatarini zaidi kuzama kutokana na ongezeko la kiwango cha maji ya bahari litokanalo na mabadiliko ya tabianchi.
UNDP Tuvalu/Aurélia Rusek
Tuvalu ambalo ni taifa la kisiwa kwenye bahari ya Pasifiki liko ukanda wa chini na hatarini zaidi kuzama kutokana na ongezeko la kiwango cha maji ya bahari litokanalo na mabadiliko ya tabianchi.
  1. Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amefanya vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kuwa moja ya vipaumbele vyake kwa kuitisha mkutano maalumu wa “Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi” utakaofanyika Septemba 23, Bwana Guterres analenga kuinua hamasa na kuhakikisha nchi zinatimiza ahadi zilizoitoa ya kupunguza ongezeko la joto duniani kama sehemu ya mkataba wa Paris wa mwaka 2015.

Mkutano huo utawaleta pamoja wadau wote zikiwemo serikali, sekta binafsi, asasi za kiraia, viongozi wa mashinani na mashirika mengine ya kimataifa ili kutoka la suluhu katika masuala sita muhimu

  • Kubadili mwelekeo wa kimataifa kuingia katika nishati jadidifu
  • Miji na mioundombinu endelevu na yenye mnepo
  • Kilimo endelevu
  • Udhibiti wa misitu na baharí
  • Mnepo na kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi
  • • Utaratibu wa fedha za umma na binafsi kwa uchumi wa jumla.

Katibu Mkuu amewapa changamoto viongozi hao wa dunia kuja kwenye mkutano na mipango madhubuti na sio hotuba tu, na anatarajia mkutano huo kudhihirisha mabadiliko makubwa katika uchumi ulio mbali na mafuta na kuelekea nishati safi, na vyanzo vya nishati adidifu.”Ninataka kusikia kuhusu jinsi gani tutazuia ongezeko la hewa chafuzi ifikapo 2020 na kupunguza kwa kiasi kikubwa gesi chafuzi ya viwandani  hadi sufuri ifikapo katikati ya karne hii.

Kwa kutambua kwamba vijana wanatia shinikizo kubwa la kuchukua  hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika ajenda ya kimataifa “mkutano wa vijana wa mabadiliko ya tabianchi” utafanyika Septemba 21 ambao utakuwa kama jukwa la bvijana wakereketwa, wabunifu na wajasiriamali , ambao wanasukuma gurudumu la hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi , kuonyesha suluhu zao kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa na kukutana na wafanya maamuzi wa kimataifa.

 

2 .Kufanya huduma ya afya kwa wote kuwa hali halisi

Ripoti kuhusu hali ya kiafya Afrika itatoa hali nzima ilivyo katika bara hilo.
WHO/Africa
Ripoti kuhusu hali ya kiafya Afrika itatoa hali nzima ilivyo katika bara hilo.

Siku hiyo hiyo ya mkutano wa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi , Umoja wa Mataifa utafanya mkutano wa kwanza kabisa wa ngazi ya juu kuhusu “Huduma ya afya kwa wote” ukibeba mada “Kusonga mbele kwa pamoja kujenga dunia yenye afya bora” ambapo Umoja wa Mataifa unasema utakuwa mkutano wenye umuhimu mkubwa kabisa wa kisiasa kuwahi kufanyika kuhusu huduma ya afya kwa wote.

Wakati takriban nusu ya watu wote duniani wakikosa fursa ya hudumu za msingi za afya wanazozihitaji  na gharama za afya kuwasukumu watu wapatao milioni 1000 kutumbukia kwenye umasikini uliokithiri kila mwaka, mkutano huo umeelezwa kuwa ni fursa nzuri na ya kipekee ya kuhakikisha ahadi ya kisiasa inapatikana kutoka kwa wakuu w anchi na serikali  kuweza kuweka kipaumbele na kuwekeza katika huduma ya afya kwa wote na kuhakikisha afya kwa wote.

Amesema nchi zote zimeahidi kujaribu kutimiza lengo la huduma za afya kwa wote  ifikapo mwaka 2030 ambayo inajumuisha ulinzi wa hasara za kifedha, huduma za afya za ubora wa ju una fursa  kupata dawa na chanjo muhimu zilizo salama, zinazofanya kazi, zenye ubora na za gharama nafuu.

 3 Kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)

Malengo ya maendeleo endelevu katika jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York mwaka 2015
UN Photo/Cia Pak
Malengo ya maendeleo endelevu katika jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York mwaka 2015

Ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu ambayo ni changamoto kubwa kuwahi kuchukuliwa kuibadili dunia , kuongeza mafanikio na kuhakikisha mustakabali bota kwa wote , huku tukilinda amazingira imegawanyika katika malengo 17 ya maendeleo au SDGs. Na katika malengo hayo kuna ahadi ya

  • Kutokomeza umasikini na njaa , kupanua wigo wa fursa za afya, elimu , haki na ajira.
  • Kuchagiza ujumuishi na ukuaji endelevu wa uchumi
  • Kuilinda sayari dunia kutokana na mmomonyoko wa mazingira na kupunguza athari mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano wa SDGs utafanyika Septemba 24 na 25 na utakuwa ni wa kwanza wa aina yake tangu ajenda ya maendele endelevu ilipopitishwa mwaka 2015 na ni fursa ya kusongesha mbele mchakato wa utimizaji wa malengo yote 17.

Umoja wa Mataifa umeshuhudia hatua zikipigwa katika miaka minne iliyopita lakini umeonya kwamba vita, mabadiliko ya tabianchi, ukosehu wa fursa za huduma za msingi za afya , ongezeko la pengo la usawa na pengi kubwa la ufadhili vimekuwa kikwazo kwa juhudi za kimataifa za kufikia malengo hayo. Wale walioachwa nyuma wameendelea kuathirika ikiwemo wale walio katika mataifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea (SIDS), nchi zilizo na maendeleo duni (LDCs) nan chi zisizo na bahari zinazoendelea.

4 Ufadhili kwa ajili ya maendeleo

Washiriki wa mkutano wa kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD, 2018, Addis Ababa, Ethiopia.
UNCTAD
Washiriki wa mkutano wa kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD, 2018, Addis Ababa, Ethiopia.

Hakuna lengo litakaloweza kutimizwa bila kuwa na fedha, lakini kuchangisha fedha za kutosha za ufadhili ni mtihani mkubwa.Kuongeza hatari za madeni na vikwazo vua biashara , maana yake uwekezaji ambao ni muhimu kwa kutimiza ajrenda ya 2030 hautoshelezi.

Mjadala wa ngazi ya juu kuhusu ufadhili kwa ajili ya maendeleo utakaofanyika Septemba 26 utawaleta pamoja viongozi wan chi, wafanyabiashara na sekta za fedha, kwa dhamira ya kusaka rasilimali na ushirika unaohitajika na kusongesha mbele mchakato wa maendeleo. Inakadiriwa kwamba uwekezaji wa takriban dola trilioni 5 hadi 7 unahitajika kila mwaka katika sekta zote ili kufikia malengo ya SDGs, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatoa wito wa kuweka mazingira ambayo yatawezesha uwekezaji wa muda mrefu katika maendeleo endelevu, kuchagiza afya na mustakbali wa watu wote na sayari dunia.

5 Kusaidia mataifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akiwa katika kisiwa cha Tuvalu kilichoko katika bahari ya Pasifiki.
UN Photo/Mark Garten)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akiwa katika kisiwa cha Tuvalu kilichoko katika bahari ya Pasifiki.

Mkutano wa mwisho kati ya mitango ya ngazi ya juu wakati wa UNGA74 ni tathimini ya mwelekeo wa SAMOA mwelekeo uliofikiwa miaka mitano iliyopita baada ya muafaka wa kusaidia maendeleo endelevu katika visiwa vidogo vinavyoendelea.

Visiwa hivyo ni miongoni mwa nchi zilizo na changamoto nyingi duniani zikikabiliwa na masuala yanayohusiana na kwanza udogo wa visiwa vuyao, mahali viliko, changamoto za kiuchumi na matatizo ya kimataifa ya mazingira ikiwemo athari za mabadiliko ya tabianchi.

Tathimini itajadili hatua zilizopigwa katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kukuza uchumi na mnepo wa kimazingira pamoja na changamoto zingine.

Masuala haya pia yatakusiwa kwa kila katika mikutano mingine minne ambayo itafanyika wiki hiyohiyo. Serikali, sekta binafsi, asasi za kiraia, wanazuoni, na wadau wengine watachagizwa kuanzisha ushirika mpya ambao utasonhgesha mbele utekelezaji wa vipaumbele vya mwelekeo wa SAMOA na malengo ya maendeleo endelevu katika mataifa hayo ya visiwa vidogo vinavyoendelea.