Nigeria sitisheni uhamishaji watu kwa shuruti:Leilani Farha

24 Septemba 2019

Mtaalam huru wa haki za binadamu kuhusu masuala ya haki ya makazi leo ameitaka Nigeria kuchukua hatua haraka kusitisha uhamishaji watu kwa shuruti na kushughulikia tatizo kubwa la ukosefu wa nyumba .

Katika taarifa yake iliyotolewa leo mbele ya Baraza la Haki za binadamu baada ya kurejea kutka Nigeria alikukuwa ziarani kwa siku 10, Leilani Farha amesema kuna mgogoro mkubwa wa haki za binadamu unaopaswa kushughulikiwa haraka nchini Nigeria ambao unadhihirisha hali isiyo ya kibinadamu katika makazi yasiyo rasmi. Ameongeza kuwa “Wakazi wengi wa makazi yasiyo rasmi yanayoongezeka nchini Nigeria ambayo yanahifadhi takriban asilimia 70 ya wakazi wa mijini, wanaishi bila hata fursa ya huduma za msingi kama maji ya bomba na vyoo. Hawana haki yoyote ya ulinzi wa kupanga nyumba na kutwa wanatawaliwa na hofu ya kufurushwa kutoka kwenye nyumba zao”

Bi. Farha amesema “Serikali zilizofanikiwa zimeruhusu pengo la kiuchumi Nigeria kufikia kiwango cha hatari , na ukweli ni kwamba kuna Ushahidi wa kutosha kuhusu hilo katika sekta ya nyumba. Inakadiriwa kwamba kuna upungufu wa nyumba milioni 22 na watu milioni 130 wanakosa huduma za msingi za usafi. Wakati huohuo kuna majengo mapya ya fahari yanaongezeka kama uyoga mijini ambayo mengine yamewezekana tuu kwa kuwashinikiza kuhama jamii masikini.”

Nyumba hizo hazikidhi mahitaji yopyote ya nyumba huku nyingi zikisalia tupu na kutumika kama vyombo vya utakatishaji fedha au uwekezaji ameongeza mtaalam huyo.

Mtaalam huyo pia ameelezea wasiwasi wake kwamba “ watu wanaoishi katika umasikini na kutokuwa na makazi wanasumbuliwa na kukamatwa na polisi, wanaswekwa rumande na kutozwa fini au kufungwa kwa kuzurura. Ameeleza pia watu wenye ulemavu mara nyingi wanashikiliwa katika vituo bila ridhaa yao wakiishi katika mazingira magumu sana.”

Kutokana na unyanyapaa na ubaguzi wa wamiliki wa nyumba , watu walio na virusi vya HIV na ukimwi na watu wa jamii ya mapenzi ya jinsia moja LGBT wako katika hatari kubwa ya ukiukwaji wa haki zao za nyumba, na wanawake wanakabiliwa na ukatili wa kijinsia majumbani na katika jamii na pia mara nyingi hawana pa kukimbilia kwa kuwa malazi ya dharura hayatoshi nchi nzima.

Amesema kuwa “nilishtushwa sana kuona kuwa watu ambao ndio wanaohitaji msaada zaidi na ulinzi kutoka kwa serikali  badala yake wanateswa, kubughudhiwa, kunyanyaswa, n ahata kukamatwa na kufungwa bila kutenfa makossa yoyote.”

Ameiambia serikali ya Nigeria ni lazima ichukue hatua haraka kutowaharamisha watu wasio na makazi  na watu masikini na kutangaza kusitisha nchi nzima kuwafurusha kwa nguvu katika makazi yao. Amesema hatua hizo zitasaidia kuboresha Maisha ya wale wanaohitaji msaada zaidi na zinaweza kuanza mara moja kwani hazina gharama zozote kwa serikali.

Farha atawasilisha ripoti yake ya kina ya ziara yake kwenye Baraza la haki za binadamu mwezi Machi mwaka 2020.

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter