Skip to main content

Nahimiza vijana kuendelea na vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi-Guterres

Kongamano la vijana kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
UN Photo/Kim Haughton
Kongamano la vijana kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Nahimiza vijana kuendelea na vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi-Guterres

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres leo Septemba 21 ameungana na vijana na kutoka kote ulimwenguni katika kongamano la aina yake la vijana na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Bwana Guterres akihutubia vijana hao amenaza kwa kusema, “nimekuwa mzungumzaji mara nyingi kuliko msikilizaji. Na hiyo ni moja ya changamoto za viongozi duniani: wanazunugmza sana na wanasikiliza kidogo. Na ni kaika kusikiliza ndipo tunajifunza.”

Bwana Guterres ameelezea kufurahishwa kwake na uongozi na utofauti wa harkati za vijana kwa ajili ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi duniani leo.

Katibu Mkuu huyo amesema alipoanza jukumu lake kama mkuu wa Umoja wa Mataifa alikatishwa tamaa na uwezekano wa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, na kuongeza kwamba, “tayari tunakabiliwa na dharura ya mabadiliko ya tabicnhi tunashuhudia, bila kuingia kwa undani sana, lakini tunashuhudia ongezeko la majanga ya asili yakiendelea kuwa makubwa na yenye madhara zaidi.”

Guterres ameongeza kwamba athari hizo ni dhahiri huku akitolea mifano mingi ikiwemo, “tunashuhudia ukame barani Afrika, kwa mfano katika baadhi ya matukio, sio tu inafanya jamii kutoweza kuishi lakini pia inaathiriwa na mzozo kwa mfano Sahel, ambako ukosefu wa raslimali maji inasababisha wakulima na wengine kupigana, na kwa sababu hiyo inachochea kuzuka kwa mizozo na kusambaa kwa ugaidi.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres(katikati) Wanjuhi Njoroge kutoka Kenya kulia kwake na Greta Thurnberg kutoka Sweden kushoto
UN Photo/Kim Haughton
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres(katikati) Wanjuhi Njoroge kutoka Kenya kulia kwake na Greta Thurnberg kutoka Sweden kushoto

Katibu Mkuu huyo amesisitiza umuhimu wa vijana katika kuchagiza taasisi kusukuma kufikia mchakato wa kufanya maamuzi. Akiongeza kwama  “Hatuishi katika utandawazi wenye haki, cha kushangaza ni kwamba sio bara Afrika au visiwa vidogo kwenye ukanda wa Pasifiki au Carribea, ndio wachangiaji wakubwa wa mabadiliko ya tabianchi lakini ndio waathirika wakubwa.

Na hivyo, “tunahitaji kuunganisha mabadiliko ya tabianchi na mfumo mpya wa maendeleo, mfump ambao una haki zaidi miongoni mwa watu, na uhusiano sawa kwa watu na sayari dunia.”

Bwana Guterres ameongeza kwamba, ninaamini kwamba kile vijana wanafanya hii leo, na harakati mashinani ni muhimu kuwezesha kuleta mabadiliko, nawahimiza kuendelea na pale watu wanaposema, “ni hatari au ni ngumu, tahadhari na hawa vijana, sita tahadhari, nawachagiza kuendelea.”

Bwana Guterres amehitimisha kwa kusema ana wajukuu na kwamba anataka waweze kuishi katika sayari dunia bora na kwamba, “kizazi changu kina wajibu mkubwa. Ni kizazi chenu kitakochotuwajibisha kuhakisha kwamba hatusaliti mustakbali wa binadamu.”

Wanjuhi Njoroge, mwanaharkati kijana wa mazingira kutoka Kenya na mshiriki wa kongamano la vijana kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
UNnewskiswahili/Patrick Newman
Wanjuhi Njoroge, mwanaharkati kijana wa mazingira kutoka Kenya na mshiriki wa kongamano la vijana kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

 Baadhi ya vijana ambao waliungana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni Wanjuhi Njoroge kutoka Kenya akiwakilisha vijana kutoka Afrika amesema,  ‘katika juhudi zetu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kama wachangiaji wadogo wa uchafuzi wa mazingira na waathirika wakubwa, lakini sasa sio wakati wakunyosheana kidole ni wakati wa kufanya kazi pamoja, sisi vijana takriban milioni 625 kutoka Afrika tunoamba uungwaji mikono katika ufundi, kifedha na kubadilishana ujuzi Na stadi Katika hatua dhidi ya kukabiliana na kuzuia mabadiliko ya tabianchi. Mapema wiki hii Idhaa ya Kiswahili imezungumza na Wanjuhi ambaye ameelezea ujumbe wake kwa Umoja wa Mataifa.

Kongamano hili la vijana limefanyika siku chache kabla ya kongamano la Katibu Mkuu la kuchagiza viongozi wa dunia kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi Septemba 23.