Nakaribisha uamuzi wa Rais wa Cameroon kuanzisha majadiliano ya kitaifa:Guterres

11 Septemba 2019

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha tangazo la rais Paul Biya wa Cameroon la kuanzisha mchakato wa majadiliano ya kitaifa.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake jumanne, Bwana Guterres ameichagiza serikali ya Cameroon kuhakikisha kwamba mchakato huo unakuwa jumuishi na kushughulikia changamoto zinazolikabili taifa hilo la afrika ya Magharibi.

Katibu Mkuu pia ametoa wito kwa wadau wote nchini Cameroon wakiwemo wanaoishi ughaibuni, kushiriki katika juhudi hizo.

Pia amerejelea kuhimiza kwamba Umoja wa Mataifa uko tayari kuisaidia Cameroon katika mchakato huo wa kitaifa wa majadiliano.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud