Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila nchi ina wajibu wa kulinda watu dhidi ya mashambulizi ya chuki:Bachelet

Rabbi Yisroel Goldstein,wa Sinagogi la Chabad Powey mjini California akizungumza wakati wa tukio maalumu la kukabiliana na chuki dhidi ya Wayahudi na mifumo mingine ya ubaguzi wa rangi na chuki
UN Photo/Manuel Elías
Rabbi Yisroel Goldstein,wa Sinagogi la Chabad Powey mjini California akizungumza wakati wa tukio maalumu la kukabiliana na chuki dhidi ya Wayahudi na mifumo mingine ya ubaguzi wa rangi na chuki

Kila nchi ina wajibu wa kulinda watu dhidi ya mashambulizi ya chuki:Bachelet

Haki za binadamu

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ameongeza sauti yake katika kulaani mashambulizi ya risasi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki nchini Marekani na kusisitiza kwamba sio Marekani tu bali mataifa yote yanapaswa kufanya juhudi zaidi kukomesha ubaguzi.

Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Geneva Uswis hii leo msemaji wa Kamishina huyo Rupert Colville amekaribisha ya Marekani ya kulaani ubaguzi wa rangi, chuki na dhana ya kuona kwamba watu weupe ni bora zaidi yaw engine, baada ya mashambulio mawili ya kusikitisha yaliyokatili maisha ya watu 29 jimboni Texas na Ohio siku ya Jumamosi.

Collvile ameongeza kuwa “Tunalaani vikali ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na kutovumiliana ikiwemo dhana ya kufikiria watu weupe ni bora zaidi yaw engine, na tunatoa wito kwa mataifa yote sio Marekani tu kuchukua hatua kutokomeza ubaguzi.”

Wito huo unaunga mkono ule wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alioutoa kufuatia mashambulizi hayo ya risasi nchini Marekani ambapo alionyesha mshikamano na watu na serikali za Marekani na Mexico kufuatia mauaji hayo na majeruhi wa El Paso.

 Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet
ILO/M. Creuset
Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet

Kuhusu msimamo wa Rais wa Marekani

Alipoulizwa endapo mtazamo wa Rais Donald trum dhidi ya wageni unaweza kuwa chachu ya mashambulio hayo ya karibuni bwana Colville alijibu kwamba mamlaka zote zinapaswa kuhakikisha kwamba hatua zinazochukua hazichangii kwa aina yoyote ile tabia ya watu katika jamii ambayo ni ya kibaguzi au inayonyanyapaa, au kuwachukia walio wachache. Na wachache hao ni pamoja na wakimbizi, wahamiaji, wanawake, LGBT, au wengineo, na endapo mamlaka hazitochukua hatua Madhubuti kundi hili litaendelea kuwa katika hofu ya kmashambulizi.

Kuhusu maelezo ya Trump kwamba sheria mpya inaweza kujumuisha hukumu ya kifo kwa uhalifu wa chuki na mashambulizi ya risadi kwa watu wengi , Bwana Colville amesisitiza kuwa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inapinga hukumu ya kifo katika mazingira ya aina yoyote ile na kwamba hukumu hiyo haina nafasi katika karne ya 21. Ameongeza kuwa uhalifu wa chuki unapaswa kushughulikiwa pamoja na chanzo chake , lakini sharia mpya zinahitaji kuwa makini pia na kutilia maanani uhuru na haki za binadamu.

Na kuhusu endapo watu wente matatizo ya akili ndio walihusika na mashambulizi hayo, Collvile amemnukuu Kamisha mkuu wa haki za binadamu aliyeondoka , Zeid Ra’ad Al Hussein, aliyesema kwamba “Ni vigumu kupata kitu kinachohalalisha maelezo rahisi kwamba ni watu gani wanaweza kununua silaha zikiwemo za hatari , licha ya historia zao za uhalifu, matumizi ya mihadarati, ukatili wa kijinsia na matatizo ya akili au mahisiano ya moja kwa moja na magaidi wa ndani na nje.”

Pia bwana Colville ameyataka makampuni ya mawasiliano na serikali kushirikiana kuhakikisha kwamba wanazingatia masuala ya haki za binadamu wanaoandaa sharia, sera na vitu vitakavyotumika katika miatandao ya kijamii ili kusaidia kubaini na kupunguza hatari.