Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huhitaji kuwa na kitu kuwakirimu wengine, moyo wako tu-Msanii Djamal 

Picha iliyochorwa na mtoto wa miaka 10 kutoka Ureno na kuingia katika fainali za shindano la kimataifa la sanaa la watoto kuhusu haki za binadamu 2018
UNOG
Picha iliyochorwa na mtoto wa miaka 10 kutoka Ureno na kuingia katika fainali za shindano la kimataifa la sanaa la watoto kuhusu haki za binadamu 2018

Huhitaji kuwa na kitu kuwakirimu wengine, moyo wako tu-Msanii Djamal 

Msaada wa Kibinadamu

Kusaidia mtu si lazima uwe na kitu na ndio maana wahenga walinena “kutoa ni moyo na usambe si utajiri”Kauli hii inazingatiwa na msanii wa uchoraji Djamal Ntagara wa nchini Rwanda ambaye ameamua kufungua nyumba yake na kutumia taaluma yake kuwakirimu wengine hususan wakimbizi. Jason Nyakundi na maelezo zaidi

Hiyyo ni sauti ya msanii Djamal akisema kwa hakika huitaji kuwa na kitu kumsaidia mtu bali moyo wako tu wa ukarimu. Na moyo wake ndio uliomfanya afungua mlango wa nyumba yake kwa wasanii wote wanaotaka kujifunza uchoraji akiwemo Mike Katihabuka aliyekimbia Burundi mwaka 2015. Mike aliishi kwenye kambi ya wakimbizi kwa muda na kisha akaenda mjini Kigali alikopata fursa ya kukutana na Djamal

(SAUTI YA MIKE KATIHABUKA )

Rwanda inahifadhi wakimbizi 150,000 na 13, 000 kati yao wanaishi mijini ikiwemo Kigali ambako wanaweza kufanya kazi na kujitegemea. Kwa msaada wa Djamal Mike ameweza kuendelea kufanya kazi ya usanii wa kuchora anayoihusudu sana na wamekuwa zaidi ya marafiki kama ndugu

(SAUTI YA DJAMAL )

“Kila mtu lazima amchukulie mkimbizi kama kaka, kama jirani , kama ndugu na sio mtu baki”

Na ndivyo alivyomchukulia Mike

(SAUTI YA MIKEKATIHABUKA )

Na sasa marafiki hao wanafanya maonyesho yao ya picha pamoja kipato wanachopata kutokana na picha hizo kinawawezesha kusaidia familia zao. Mbali ya ukarimu wa Djamali wawili hawa wana kitu mahsusi kinachowaunganisha ambacho ni sanaa.