Bei ya chakula imepungua kidogo mwezi Julai-FAO

Mkulima na mpunga baada ya mavuno Bangladesh.FAO yasema bei ya nafaka ilipanda kwa asilimia 4.0 mwezi Agosti.
Picha: IFAD/GMB Akash
Mkulima na mpunga baada ya mavuno Bangladesh.FAO yasema bei ya nafaka ilipanda kwa asilimia 4.0 mwezi Agosti.

Bei ya chakula imepungua kidogo mwezi Julai-FAO

Ukuaji wa Kiuchumi

Bei ya chakula imepungua kidogo mwezi Julai kufuatia kushuka kwa bei ya nafaka, bidhaa zitokanazo na maziwa na sukati ikilinganishwa na bei za juu za nyama na mafuta.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la chakula duniani, FAO, makadirio ya bei ya chakula vipimo vya bidhaa tano vya vyakula katika soko la bidhaa ilifikia wastani wa pointi 170.9 mwezi Julai mwaka 2019 ma kushuka hadi asilimia 1.1 chini ya viwango mwezi Juni lakini na kufika asilimia 2.3 ikilinganishwa na mwaka jana.

Bei ya nafaka

Bei ya nafaka ilishuka kwa asilimia 2.7 ikilinganishwa na mwezi Juni lakini ni asilimia 4.1 juu ya viwanngo mwaka jana mwezi Julai. Kushuka kwa bei kukichangiwa na kushuka kwa bei za ngano na mahindi ikiashiria mauzo ya nje ya juu tofauti na mchele ambao bei yake ilisalia thabiti licha ya kupungua kwa mauzo.

Bei ya mafuta

Bei ya mafuta yatokanayo na mimea iliongezeka kwa asilimia 0.8 mwezi Julai ikiongozwa na bei ya juu ya mafuta kutokana na mafuta ya soya na alzeti licha ya kushuka kwa bei ya mafuta ya mawesehii ikitokana na mazao ya juu kusinimashariki  ikijumuishwa na kupungua kwa mahitaji ya bidhaa katika soko la kimataifa.

Bei ya nyama

Bei ya nyama imeongezeka kwa asilimia 0.6 kutoka kwa viwango vya Juni hii ikiwa ni mwezi wa sita wa kushuhudia kupanda kwa bei.

Bei ya nyama ya kondoo na ng’ombe iliongezeka mwezi Jul;ai kufuatia kuongezeka kwa mahitaji kutoka Asia na kukosekana kwa bidhaa hiyo kutoka Oceania. Kwa upande mwingine bei ya nyama ya nguruwe ilishuka baada ya miezi minne ya kuendelea kupanda, ikiashiria upatikanaji wa bidhaa za mauzo ya nje kutoka Brazil na Marekani.

Bei ya bidhaa za maziwa

Bei ya bidhaa za mwaziwa ilipungua kwa asilimia 2.9 kutoka Juni ikiashiria kushuka kwa bei kwa mwezi wa pili mfululizo kufuatia kushuka kwa be iza siagi na jibini na maziwa ya unga.

Bei ya sukari

Bei ya sukari ilipungua kwa asilimia 0.6 ikilinganishwa na mwezi Juni kufuatia mtarajio ya mazao ya juu ya miwa nchini India ambayo ni mzalishaji mkubwa wa sukari. Kushuka kwa bei ya sukari pia kulichangiwa na kuimarika kwa Real ya Brazil dhidi ya dola ya kimarekani suala ambalo mara nyingi huathiri mauzo ya nje ya sukari kutoka Brazil ambayo ni muuzaji mkubwa wa sukari nje.