Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yakaribisha uwezekano wa kuanza mazungumzo baina ya Marekani na DPRK

Rais wa Marekani Donald Trump akishikana mkono na Rais Kim Jong-un wakati viongozi hao wawili walipokutana katika eneo lisilo na majeshi likizitenganisha Korea kaskazini na kusini (30 Juni 2019)
White House/Shealah Craighead
Rais wa Marekani Donald Trump akishikana mkono na Rais Kim Jong-un wakati viongozi hao wawili walipokutana katika eneo lisilo na majeshi likizitenganisha Korea kaskazini na kusini (30 Juni 2019)

UN yakaribisha uwezekano wa kuanza mazungumzo baina ya Marekani na DPRK

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha  na kuunga mkono uwezekano wa kuanza tena mazungumzo baina ya serikali ya Marekani na ya Jamhuri ya watu wa Korea  au DPRK, uhusiano ambao unaweza kuchangia kuivua silaha za nyuklia nchi hiyo ya rasi ya Korea ambayo pia hujulikana kama Korea Kaskazini.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Guterres amekaribisha “mikutano iliyofanyika Panmujom baina ya rais kim Jong-Un wa DPRK na Rais Donald Trump wa Marekani hususan tangazo lao kwamba DRP na Marekani wataanza mazungumzo ya ngazi ya kikazi.”

Kwa mara ya kwanza tangu mkutano wao kwenye mji mkuu wa Vietnam wa Hanio uliposambaratika mwezi Februari nchi zote mbili zimeafiki kuanza majadiliano kuhusu nyuklia.

Kabla ya kuvuka na kuingia kwenye mazungumzo viongozi hao wawili Trump na Jong-Un walitoa fursa kwa wapiga picha kujipatia kumbukumbu katika eneo hilo lisilo na askari wowote. Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeendelea kusema kwamba “Katibu Mkuu anaunga mkono juhudi zinazoendelea za pande zote kufufua upya uhusiano katika kuelekea amani ya kudumu, usalama na kukamilisha uvuaji wa silaha za nyuklia katika Ras ya korea.

Majadiliano baina ya Marekani na Korea Kaskazini kuhusu nyuklia yamekuwa yakiendelea kwa miongo, bila mafanikio ya kusitisha mipango ya utengenezaji wa silaha za atomiki.

Rais wa Marekani Donald Trump na Kim Jong-un wa Korea Kaskazini 30 Juni 2019 katika eneo lisilo na majeshi linalozitenganisha Korea ya kusini ya kaskazini.
White House/Shealah Craighead
Rais wa Marekani Donald Trump na Kim Jong-un wa Korea Kaskazini 30 Juni 2019 katika eneo lisilo na majeshi linalozitenganisha Korea ya kusini ya kaskazini.

 

Mwaka 2017 Pyongyang ilirusha kombora lake la sita katika moja ya majaribio makubwa kabisa nyuklia tangu ilipoanza mpango huo mwaka 2006, hali ambayo ilizidi kuutia dosari uhusiano baina ya Marekani na DPRK katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Rais Trump.

Mwaka uliofuata Rais trump na Rais Jong-Un walikutana Singapore na kutia saini taarifa ya pamoja wakiahidi kusaka amani na kukamilisha upokonyaji wa nyuklia kwenye rasi ya Korea.

Wawili hao walikutana tena Februari 2018 , lakini kutofautiana kuhusu vikwazo na uvuaji wa silaha za nyuklia kulifanya mkutano wao kusambaratika mapema na bila kuzaa matunda yoyote.