Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumalizika kwa hatua ya usitishaji majaribio ya nyuklia DPRK kwanitia hofu:Guterres

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akizungumza na wanahabari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
UN Photo/Cia Pak
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akizungumza na wanahabari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Kumalizika kwa hatua ya usitishaji majaribio ya nyuklia DPRK kwanitia hofu:Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amesema ana wasiwasi mkubwa na kumalizika kwa hatua ya usitishaji wa majaribio ya makombora ya nyuklia nchini Jamuhuria ya watu wa Korea au DPRK.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Januari Mosi mjini New York Marekani Guterres amesema duru za habari zimeripoti kwamba kiongozi wa DPRK Kim Jong-un ametangaza kwamba nchi yake ambayo pia hujulikana kama Korea Kaskazini haifungwi ten ana marufuku iliyojiwekea ya kusitisha majaribio ya makombora ya nyuklia.

Kujihusisha kidiplomasia ndio njia pekee ya amani endelevu-Antonio Guterres.

Katibu Mkuu amesisitiza kwamba “natumai majaribio hayataanza tena kwa kuzingatia maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa”

Taarifa yake imeongeza kwamba “Kutozalisha silaha za nyuklia kunasalia kuwa ngunzo muhimu ya kimataifa ya usalama wa nyuklia na inapaswa kuheshimiwa.”

Katibu Mkuu pia amerejelea kusisitiza msaada wake kwa kuanza majadiliano yenye lengo la kukamilisha na kuthibitisha uvuliwaji wa silaha za nyuklia kwenye rasi ya Korea.