Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Filamu imenitoa hofu, sasa watu wengi wanafahamu shida zetu- Lazarus

Mahojiano na Mwanamuzi Lazarus Chigwandali  kutoka Malawi ambaye ni mlemavu wa ngozi
UN /Mark Garten
Mahojiano na Mwanamuzi Lazarus Chigwandali kutoka Malawi ambaye ni mlemavu wa ngozi

Filamu imenitoa hofu, sasa watu wengi wanafahamu shida zetu- Lazarus

Haki za binadamu

Lazarus Chigwandali, mmoja wa watu wenye  ualibino kutoka Malawi ambaye sasa anatumia kipaji chake cha ameomba kuwepo kwa mfuko wa kujengea uwezo watu wenye ulemavu wa ngozi barani Afrika ili waweze kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi na hatimaye kujiongezea kipato na kujikwamua kimaisha. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

 Ndani ya studio za Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Lazarus akicheza gitaa alilojitengenezea wakati akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, kufuatia filamu iitwayo Lazarus, iliyotengenezwa ikimulika maisha yake nchini Malawi, nchi ambayo mauaji dhidi ya kundi hili yametishia uhai wao. Lazarus anasema, “kila siku nina hofu kwa sababu nchini Malawi watu wenye ualibino wanauawa kwa sababu ya viungo vyao, kwa hiyo hafahamu nani amuamini au aende wapi.?”

Lazarus ambaye naye ana watoto wawili wote wenye  ulemavu wa ngozi ana anapata kipato kwa kuburudisha watu mitaani kwa gitaa lake lifananalo na banjo, anasema hivyo filamu Lazarus imekuwa ni ufunguo kwake kwa kuwa, “kwa kuwa filamu imeshatoka, dunia nzima itafahamu kinachoendelea kwa watu kama  yeye Malawi na barani Afrika. Inaonekana watu wengi hawafamu hiki kinachoendelea.”

 Na filamu imemshawishi kuzungumza zaidi kwani awali alikuwa na hofu na hakuwa na jukwaa na ujumbe wake kwa Umoja wa Mataifa na  jamii ya kimataifa ni kwamba, “nausihi Umoja wa Mataifa kwa sababu una nguvu ya kuleta mabadiliko na uiambie Malawi itusaidie zaidi na ihamasishe watu kuelewa kuwa sisi pia ni watu.”

 Na kuhusu ni usaidizi gani wanataka, Lazarus anasema kuanzishwe mfuko maaalum wa kuwajengea uwezo wa kiuchumi ili hatimaye wafungue hata biashara akisema yeyé binafsi, “natamani kuwa na mashine ya kusagisha mahindi, au duka la bidhaa ndogo ndogo kwa kuwa pale ninapotoka watu wanasafiri mbali kupata bidhaa.”