Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajira kwa watoto hutumbukiza nyongo ndoto zao

Watoto na watu wazima kutoka Romania wakifanyakazi katika eneo la kutupa taka jirani na makazi ya Nadezhda nchini Bulgaria. Familia hizi zinakosa fursa za ajira, ambayo ndio kauli mbiu ya ripoti ya mwaka huu ya ILO kuhusu mtazamo wa ajira na mwenendo Duni
UNICEF
Watoto na watu wazima kutoka Romania wakifanyakazi katika eneo la kutupa taka jirani na makazi ya Nadezhda nchini Bulgaria. Familia hizi zinakosa fursa za ajira, ambayo ndio kauli mbiu ya ripoti ya mwaka huu ya ILO kuhusu mtazamo wa ajira na mwenendo Duni

Ajira kwa watoto hutumbukiza nyongo ndoto zao

Haki za binadamu

 

Shirika la Chakula na Kilimo FAO limetoa wito kwa nchi zote kuungana na kutenga fedha zaidi kukabiliana na ajira ya watoto katika sekta ya chukula na katika kilimo cha kujikimu ambapo kiwango kikubwa cha ajira za watoto hushuhudiwa.

Wito huo wa kutaka hatua kuchukuliwa ulitolewa wakati FAO inaadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ajira za watoto kwenye mkutano wa kimataifa ambao shirika hilo liliuandaa kwa ushirikiano na mkuu wa Tume ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo na shirika la kazi ulimwenguni ILO mjini Brussels Ubelgiji.

“Ni wakati wa kuwekeza fedha zaidi katika kupambana na ajira za watoto katika nyanja zote,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa  FAO José Graziano da Silva kwa njia ya ujumbe wa video uliorekodiwa kwa minajili ya Siku ya Kimataifa ya Mwaka ya kupinga ajira ya watoto.

Graziano da Silva pia aliazungumzia wajibu muhimu katika vugu vugu la ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na tatizo la ajira za watoto katika kilimo, lililoanzishwa na mashirika ya ILO, FAO na washirika wengine. “Kwa pamoja tunweza kuwa na mabadiliko mkubwa, na maisha bora ya baadaye ya watoto wetu,” alisema.

Hitaji la kufahamu chanzo cha ajira za watoto.

Kati ya watoto milioni 152 walio katika ajira za watoto kote duniani, zaidi ya asilimia 70 au wasichana milioni 108 na wavulana kati ya miaka 5 na 17 hufanya kazi katika kilimo, sekta mifugo, sekta ya misitu na kilimo cha samaki. Idadi ya watoto watoto katika ajira za watoto imeongezeka kwa milioni kumi tangu mwaka 2012. Asilimia 85 ya ajira za watoto barani Afrika hupatikana  katika sekta ya kilimo.

Baadhi ya masuala makuu yanayochangia ajira za watoto katika sehemu za vijijini ni pamoja na kipato cha chii cha familia na umaskini nyumbani, tegemeo kidogo katika maisha, elimu duni na utekelezwaji mbana ya wa sheria za ajira.

Ajira ya watoto ni nini?

Ajira ya watoto ni kazi ambayo mtoto hastahili kuifanya kwa umri wake, ambayo humzuia mtoto kupata elimu, au inayoweza kuathiri afya yao, usalama wao na tabia.

Lakini Mkurugenzi Mkuu  wa FAO alisema kuwa sio ushirika wote wa watoto unaoweza kutajwa kuwa ajira ya watoto.  Kwa mfano wasichana na wavulana wanapojifunza jinsi ya kukuza mboga au kulisha kuku katika familia zao, inaweza kuwaongezea maarifa na kuboresha maisha yao ya baadaye, alisema.

“Hata hivyo wakati watoto wanapofanya kazi saa nyingo kwa siku, wakati wanafanya kazi nzito, wakati wanafanya majukumu ambayo ni hatari kwa umri wao, wakati hii inatatiza masomo yao, hii ni ajira ya watoto, na inastahili kuangamizwa,” alisisitiza.