Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita na majanga vyachochea upya ongezeko la ajira ya watoto:FAO

Nchini Malawi, watoto wanafanya kazi katika eneo la ujenzi
ILO/Marcel Crozet
Nchini Malawi, watoto wanafanya kazi katika eneo la ujenzi

Vita na majanga vyachochea upya ongezeko la ajira ya watoto:FAO

Haki za binadamu

Baaada ya miaka mingi ya kupungua, sasa ajira ya watoto katika kilimo imeanza kuongezeka tena ikichochewa na migogoro na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yameelezwa leo na shirika la chakula na kilimo FAO , katika kuadhimisha siku ya kupinga ajira kwa watoto duniani na kusema mwenendo huu hautishii tu mustakhbakli wa mamilioni ya watoto, bali pia unatishia juhudi za kutokomeza njaa na umasikini duniani.

Watoto milioni 73 wanatumikishwa katika kazi hatari

Kwa mujibu wa FAO siku ya mwaka huu inajikita kwa watoto milioni 73 kote duniani wanaoshiriki kazi zinazohatarisha afya na usalama wao, iwe ni katika shughuli za uvuvi, kilimo, kukausha samaki kwa moshi,  kazi za kuchomelea magari zinazowaweka watoto hao katika hatari kubwa.

Jacqueline Demeranville ni afisa wa FAO anayehusika na ajira zenye hadhi vijijini

“Ushirikishaji wa watoto katika kazi zenye madhara ni ukiukawaji dhahiri wa haki zao, pia kuna athari za muda mrefu za mustakhbali wao , ajali moja tu inaweza kusambaratisha uwezekano wa kipato katika maisha yao yote , hivyo tunapoteza miaka mingi ya uzalishaji, uwekezaji katika elimu na mafunzo bila kuasahau athari binafsi”

Kuhusu athari hizo amesema

“Watoto sio vijana, miili na ubongo wao bado vitnakua na hivyo kuwaweka hatarini zaidi kwa madawa kama ya kilimo na pia wanakuwa na kiwango kikubwa cha kujeruhiwa kuliko wafanyakazi watu wazima , hivyo ulinzi maalumu unahitajika”

Hata hivyo amesisitiza kuwa

Kipato kizuri na maisha yenye mneno kutawezesha wazazi kuwapeleka watoto wao shuleni badala ya kazini, pia tunahitaji kuhakikisha shule na mafunzo vipo katika maeneo yote na tunahitaji kufanya kazi na familia zinazojihusisha na kilimo, masula ya misitu na uvuvi ili kuelimisha zaidi kuhusu hatari zinzowakabili watoto na hatua za kuweza kuwalinda.”

Kijana akiwa amebeba gunia la chupa za plastiki La Paz, Bolivia.
ILO/Marcel Crozet
Kijana akiwa amebeba gunia la chupa za plastiki La Paz, Bolivia.

FAO inasema idadi ya watoto walio katika ajira ya kilimo kote duniani imeongezeka kutoka milioni 98 na kufikia milioni 108 mwaka 2012,  chachu kubwa ikitajwa kuwa ni vita, mabadiliko ya tabia nchi na uhamiaji wa shuruti.