Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ni tete kutokana na mabadiliko ya tabianchi duniani:WMO Ripoti 

Familia huko nchini Burkina Faso ikienda kusaka maji. Nchini humo zaidi ya watu 950,000 hawana uhakika wa chakula kutokana na mabadiliko ya tabianchi yaliyosababisha ukame na hivyo kukwamisha shughuli za kilimo na ufugaji.
OCHA/Otto Bakano
Familia huko nchini Burkina Faso ikienda kusaka maji. Nchini humo zaidi ya watu 950,000 hawana uhakika wa chakula kutokana na mabadiliko ya tabianchi yaliyosababisha ukame na hivyo kukwamisha shughuli za kilimo na ufugaji.

Hali ni tete kutokana na mabadiliko ya tabianchi duniani:WMO Ripoti 

Tabianchi na mazingira

Dalili za wazi na athari za kiuchumi na kijamii zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi zinazongezeka kote duniani kukishuhudiwa kiwango kikubwa cha hewa chafuzi ya viwandani inayosababisha ongezeko la joto na kufikia viwango vya hatari, kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO.

Ripoti hiyo ya WMO ya maadhimisho ya 25 “ya hali ya hewa duniani kwa mwaka 2018 inatanabaisha rekodi ya kupanda kwa kin cha bahari pamoja na ongezeko kubwa la joto baharini nan chi kavu kwa miaka minne mfululizo iliyopita. Mwenendo huu wa ongezeko la joto ukekuwepo tangu mwanzo wa karne hii na unatarajiwa kuendelea. Akisisitiza hilo mkurugenzi mkuu wa WMO Petteri Taalas amesema “Tangu kuchapishwa kwa taarifa ya kwanza sayansi ya hali ya hewa imefanikiwa kuwa na viwango vya kupindukia,vikidhihirisha kwamba kiwango cha joto duniani kinaongezeka na kuambatana m na matukio kadhaa kama vile kupanda kwa kina cha bahari, kuyeyuka kwa barafu baharini, kutoweka kwa theluji kwenye nchi ya dunia na matukio ya joto la kupindukia”

Ameongeza kuwa dalili hizi za mabadiliko ya tabianchi zinazidi kuwa bayana kila uchao kwa mfano viwango ya hewa ukaa ilikuwa ni 357.0 kwa milioni ilipotolewa ripoti ya kwanza mwaka 1993 na imeongezeka na kufikia 405.5 kwa milioni mwaka 2017 na kwa mwaka 2018-2019 viwango hivyo vya hewa ukaa vinatarajiwa kuongezeka zaidi.

WMO inasema ripoti hii imekusanya kutoka kwa mashirika ya utabiri wa hali ya hewa duniani, huduma za masuala ya maji, wataalamu wa jumuiya ya sayansi na mashjirika ya Umoja wa Mataifa na inaelezea kwa kina athari za mabadiliko ya tabianchi kwa afya ya binadamu na mustakabali wake, uhamiaji na watu kutawanywa, uhakika wa chakula, mazingira, bahari, na mfumo mziama wa Maisha duniani, lakini pia imeorodhesha matukio mbaya zaidi ya hali ya hewa duniani.

 

Hali halisi

Mwaka wa 2019 umeendelea kushuhudia hali mbaya ya hewa amesema taalas akitolea mfano kimbunga IDAI cha hivi karibuni ambacho kimesababisha mafuriko na uharibifu mkubwa nchini Msumbiji, Zimbabwe na Malawi. Kwa mujibu wa WMO kimbunga hicho kinaweza kuwa ni moja ya majanga hatari ya asili yaliyokatili maisha ya watu wengi kuwahi kutokea Kusini mwa Afrika.

Mwanzoni mwa mwaka huu pia kumeshuhudiwa majira ya baridi kali iliyovunja rekodi barani Ulaya , baridi isiyo ya kawaida Amerika Kaskazini na joto la kupindukia nchini Australia huku Arctic na Antactic barafu inayeyuka kwa kiwango kisicho cha kawaida.

Hofu ya mabadiliko ya tabianchi

Takwimu zilizotolewa na ripoti hiyo ndizo zinazozusha hofu kubwa kwani zinasema miaka minne iliyopita ndiyo imevunja rekodi duniani kwa kuwa kiwango cha juu cha joto ambacho kwa 2018 ni takribani nyuzi tojo 1c zaidi ya iliyokuwa kabla ya zama za maendeleo ya viwanda huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antoniuo Guterres akiandika katika ripoti hiyo kwamba “hakuna tena muda wa kusibiri wala kuchelewa" na meamua ataitisha mkutano wa kimataifa wa ngazi ya juu Septemba 23 mwaka huu na ripoti hii ya WMO itakuwa moja ya mchango kwenye mkutano huo wa wakuu w anchi na serikali za dunia.

Athari za mabadiliko ya tabianchi duniani

 

Akizungumzia ripoti hiyo Rais wa Baraza Kuu Maria Fernanda Espinosa amesema “kipaumbele changu ni mabadiliko ya tabianchi na hasa kuelezea athari zake katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu , SDG’s n ahaja ya kuelewa athari zake za kiuchumi na kijamii katika nchi zote duniani na hivyo ripoti hii itakuwa na mchango mkubwa katika juhudi zetu za pamoja kama jumuiya ya kimataifa katika kujikita kushughulikia tatizo hili.”

Athari za mabadiliko ya tabianchi kwa mujibu wa mashirika

Majanga: Kwa mwaka 2018 majanga ya asili ambayo yaliathiri watu milioni 62 yalikuwa yanahusiana na hali mbaya ya hewa na matukio ya hali ya hewa  ambapo mafurikoi yameathiri watu zaidi ya milioni 35 katika matukio 281 yaliyorekodiwa na shirika la umoja wa mataifa la upunguzaji wa athari za majanga UNISDR. Vimbunga Florence na Michael ni miongoni mwa janga yaliyogharimu mabilioni ya dola 2018 nchini Marekani na vifo zaidi ya 100. Nalo joto la kupidukia liligharimu maisha ya watu zaidi ya 1600 Ulaya, Japan na Marekani  na pia kuchangia hasara za kiuchumi za dola bilioni 49. Tyfoon huko Ufilipino iliathiri watu milioni 2.4 na kukatiza maisha ya watu 134.

Uhakika wa chakula:Hali mbaya ya hewa imeathri pakubwa sekta ya kilimo na kutishia mafanikio na hatua zilizopigwa katika kutokomeza utapiamlo.Ambapo ukame na el Nino ya mwaka 2016-2017 imesaidia kuongeza namba wya wenyeutapiamlo hadi kufikia milioni 821 duniani kote.

 

Picha ya sayari ya dunia kutumia sateliti. Mabadiliko ya tabianchi yanaiweka hatarini dunia na viumbe vilivyomo.
NASA
Picha ya sayari ya dunia kutumia sateliti. Mabadiliko ya tabianchi yanaiweka hatarini dunia na viumbe vilivyomo.

Watu kutawanywa:Kati ya watu milioni 17.7 ambao ni wakimbizi wa ndani kote duniani , zaidi ya milioni 2 kati yao walifungasha virago 2018 kwa sababu zinazohusiana na majanga yanatokanayo na mbadiliko ya hali ya hewa ikiwemo, ukame, mafuriko, na vimbunga.

Athari kwa mazingira: Mabadiliko ya tabianchi yamesababisha athari nyingi kwa mazingitra ikiwemo kubabuka kwa matumbawe, kupungua kwa hewa ya oxjeni, kupotea kwa maliaasili ya baharini kama mikoko na hata kutoweka kwa aina za samaki. Na kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP, mabadiliko ya tabianchi yamekuwa ni tishio kubwa la mfumo wa maisha kwa sababiu yameongeza athari za ukame na kuchochea hatari ya moto wa nyikani.

Ripoti hiyo imetoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka na za pamoja kudhibiti ongezeko la joto duniani, kuhifadhi mazingira na kujenga mnepo wa kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.