Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Eritrea na raia wa Ethiopia watangamana na hili ni jambo jema- Priyanka

Gur Deng Kuarban, mkimbizi kutoka Sudan Kusini, akisikiliza dadake akisoma katika kambi ya Kule nchini Ethiopia kupitia mradi wa “We love reading”.
We Love Reading
Gur Deng Kuarban, mkimbizi kutoka Sudan Kusini, akisikiliza dadake akisoma katika kambi ya Kule nchini Ethiopia kupitia mradi wa “We love reading”.

Wakimbizi wa Eritrea na raia wa Ethiopia watangamana na hili ni jambo jema- Priyanka

Wahamiaji na Wakimbizi

Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF Priyanka Chopra Jonas ametembelea Ethiopia ambako amekutanana watoto wakimbizi waliokimbilia nchini humo kutokanana majanga vita na kibinadamu yanayoendelea kwenye nchi zao. Grace  Kaneiyana ripoti kamili.

Wakati wa ziara hiyo, Priyanka alikutana na watoto na vijana wanaoishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Bambasi nchini Ethiopia, ambako kuna wakimbizi 17,000,wengi wao wakitoka Sudan, halikadhalika kambi za Hitsats za Adi-Harush ambako wanaishi wakimbizi 55,000 kutoka Eritrea.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasema Ethiopia inahifadhi wakimbizi 900,000, na hivyo kuwa nchi ya pili barani Afrika kwa kuhifadhi idadi kubwa ya wakimbizi, wengi wao wakitoka Somalia, Sudan Kusini, Eritrea, Yemen na Sudan.

Miongoni mwa wakimbizi aliokutana na katika shule ya wakimbizi kambini Bambasi ni Zulfa Ata Ey mwenye umri wa miaka minane, akiwa miongoni mwa wanafunzi 6,000 waliosajiliwa kwenye shule hiyo.

Zulfa yuko darasa la pili na ingawa darasa lake limejaa kupita kiasi, bado ana nia  ya kujifunza ili ashike nafasi ya juu akiwa na nia ya kuwa mwalimu ili asaidie watoto wengine.

Idadi ya madarasa ni chache, halikadhalika walimu na vitabu lakini hawakati tamaa kama anavyoelezea Priyanka.

(Sauti ya Priyanka Chopra Jonas)

 “Imefurahisha sana kuona jinsi hawa watoto wanaishi kwenye umaskini uliopindukia lakini bado wana furaha na ari ha kusoma. Kuna umuhimu mkubwa kufadhili huduma ya afya kwa watoto hawa ili waweze kuhitimu masomo yao. Hatutaki utoro wowote unatakiwa na hata ndoa kwenye  umri mdogo itakuwa ni jambo kubwa.”

Akiwa kwenye kambi za Hitsats na Adi-Harush, balozi mwema huyu alishuhudia huduma za shule, afya na nyinginezo muhimu ambazo zinatumiwa kwa pamoja an wakimbizi kutoka Eritrea na raia wa Ethiopia.

Mathalani mechi ya mpira wa soka ikijumuisha wacheza wakimbizi na raia ambapo manahodha wa timu mbili hizo walielezea awali jinsi ilikuwa vigumu kutangama lakini sasa wanashirikiana.

UNICEF imetoa wito kwa serikali duniani kusaidia wakimbizi na wasaka hifadhi kwa kupitisha sera bora zinazoshughulikia visababishi vya watoto kukimbia nchi zao na kusaidia wale wanaoshindwa kwenda shule kwenda shule.