Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyuki ni chachu kubwa katika kutimiza SDGs: Amina Mohamed

Nchini Moldova miradi ya Umoja wa Mataifa chini ya shirika lake la mpango wa maendeleo, UNDP na ubia na Muungano wa Ulaya, EU umeleta nafuu kwa kusaidiawafugaji wa nyuki kupata mazao bora
UNDP Moldova
Nchini Moldova miradi ya Umoja wa Mataifa chini ya shirika lake la mpango wa maendeleo, UNDP na ubia na Muungano wa Ulaya, EU umeleta nafuu kwa kusaidiawafugaji wa nyuki kupata mazao bora

Nyuki ni chachu kubwa katika kutimiza SDGs: Amina Mohamed

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Mchango wa nyuki ni muhimu sana katika juhudi za dunia za kutimiza malengo ya maendeleo endelevu au SDGs. Kauli hiyo imetolewa leo na naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohamed akizungumza kwenye hafla maalumu ya maalumu ya maadhimisho ya siku ya nyuki duniani yaliyofanyika leo kwenye Umoja wa Mataifa.

Bi. Mohamed amesema hakuna viumbe duniani wanaofanya kazi sana kama nyuki na hasa wanao na wachavushaji wengine katika kuhakikisha robo tatu ya mazao ya chakula duniani yanachavushwa. Ameongeza kuwa na mazao ambayo yameschavushwa vyema yamedhihirika kuwa na ladha nzuri na kuwa na virutibisho muhimu, kuwa na muonekano mzuri na kudumu kwa muda mrefu.

Zaidi ya lishe amesema mchango wa nyuki pia ni mkubwa katika masuala ya uchumi kwani “ ufugaji wa nyuki na mazao yake kuanzia asali, nta na masega ni vyanzo vikubwa vya mapato hususan kwa watu waishio vijijini . Na hilo ni la msingi sana kwetu hasa katika kutokomeza umasikini na njaa.”

 

Misitu bora na endelevu ni makazi bora ya nyuki
UNMISS/Eric Kanalstein
Misitu bora na endelevu ni makazi bora ya nyuki

Ukweli halisi kuhusu nyuki

Naibu Katibu Mkuu amesema utafiti mmoja wa kimataifa umekadiria kuwa uzalishaji wa chakula kimataifa wa kila mwaka ambao unategemea uchavushaji una thamani ya dola bilioni 500 au (nusu trilioni) kiasi ambacho ni kikubwa katika kuchangia maendeleo ya jamii.

Hata hivyo amesema licha ya mchango huo idadi ya nyuki na wachavushaji wengine imepungua kwa kiasi kikubwa. Kilimo cha kupindukia kishichozingatia mpangilio na dawa za kuua wadudu vinawaweka nyuki katika hatari kubwa. Nyuki pia wanakabiliwa na magonjwa mapya na wadudu na pia mabadiliko ya tabianchi limekuwa tishio kubwa kwa viumbe hawa.

Bi. Mohamed amesisitiza kwamba “kupungua na kutoweka kwa nyuki na wadudu wengine wa porini kuna athari kubwa kwa mfumo wa Maisha ya kimataifa na mustakabali wa binadamu. Juhudi mbalimbali za haraka zinahitajika kuwalinda nyuki porini, katika kilimo na katika makazi ya mijini.”

Amehimiza kwamba “Masharika yasisyo ya kiserikali, jumuiya za wafuga nyuki, mashirika ya utafiti na wanazuoni wana jukumu kubwa katika hili.”

Na mwisho ametoa wito kwa dunia na kwa kila mtu kwamba “suala la kutoweka kwa nyuki sio utani ni la hatarina na maadhimisho haya yamekuja katika wakati muafaka, tuna dhjamiria kuivalia njuga changamoto hii kote duniani , hivyo tushirikiane na kufanya kazi pamoja kuhakikisha kwamba wadiudu hawa wanaochapa kazi kuliko kawaida wanaweza kuishi ili mfumo wa Maisha na binadamu wanaowategemea waweze kufanya hivyo pia katika kizazi cha leo na vijavyo.”
 

Mfugaji wa nyuki
UNMISS/Eric Kanalstein
Mfugaji wa nyuki

Hatua za kuchukua kulinda nyuki

Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO kuna mambo sita ya kuzingatia ili kuwaenzi na kunusuru aisha ya nyuki.

  1. Nyuki wanaboresha lishe yetu kwa kutoa vitutubisho muhimu vinavyoimarisha mazao kama matunda kama, mbogamboga, mbegu, jamii ya njugu, kahawa, kokoa na almondi na mafuta na bila nyuki mazao haya yatatoweka

-Ili kulipa fadhilla kwa wadudu hawa , wapeni nyuki chakula wapendacho kwa kupanda mazao asilia kwenye bustani kwani nyuki na bustani ni kama pende na chanda, wanauhusiano na kutegemeana.

 

2. Nyuki wanatupa asali: Je wafahamu kuwa katika Zaidi ya aina 20,000 za nmyuki ni aina 7 pekee ndizo za nyuki wanaotoa asali? Na aina ya nyuki ya Western ndio huzalisha asali nyingi zaidi sawa na tani milioni 1.6 kila mwaka. Bidhaa hii yay a asili ni tamu sana na pia ni dawa dhidi ya bakteria na kwa vidonda. Pia ni chanzo kikubwa cha mapato kwa wafugaji na wakulima vijijini.

-Nunua asali ghafi kutoka kwa wakulima kwani wengi ndio wanaozingatia ufugaji endelevu wa asili, na unaweza kuwasaidia wakulima hao kwa kununua asali, nta, na bidhaa zingine zitokanazo na nyuki.

3. Nyuki wana maadili bora zaidi ya kazi: nyuki mmocha wa asali anaweza kutembelea takribani maua 7000 kwa siku na inahitaji maua milioni 4 ili kuzalisha kilo moja ya asali. Na nyuki hawa hufanya kazi kama timu bila kuchoka ili kusaidia kuandaa masega tayari kwa kuzalisha asali. Na kufanya kazi bila kuchoka kulichangia kuanzishwa msemo wa “unafanya kazi kama nyuki”

-Basi kwa kazi hiyo kubwa waenzi nyuki hawa kwa kuwawekea chombo cha maji, kwani baada ya kibarua hicho kigumu wanahitaji kunywa maji. Ni njia nzuri ya kuwafanya wapumzike.

4. Nyuki hufanya chakula chetu kiwe na ladha nzuri: Mazao yaliyochavushwa vyema hutoa chakula kingi, kinachofanana na matunda na mbogamboga zenye ladha nzuri. Mfano matufaa ambayo ymeharibika inamaanisha hayakuchavushwa vizuri.

-Kuwalinda viumbe hawa epuka matumizi ya dawa za kuulia wadudu, dawa za fangasi, au dawa zingine za kupulizia kwenye bustan yako, kwani madawa haya yanaweza kuwaua wavachuaji wetu na kutia sumu kwenye masega ya nyuki ambayo hatimaye yanaweza kuathri hata asali yenyewe. Jaribu kutumia njia za asili kukabiliana na wadudu.

5. Nyuki wanaongeza uzalishaji wa chakula na kuwepo kwa uhakika wa chakula:moja ya tafiti ambako uchavuaji ulikuwa unafanyika kwa mpangilio katika kundi dogo la wakulima mazao yaliongezeka kwa asilimia 24 hivyo nyuki na wachavuaji wengine wanaboresha Maisha ya wakulima wadogo wadogo bilioni 2 duniani kote ambao wanasaidia kuhakikisha uhakika wa chakula .

-La kufanya sasa ni kutengeneza mazingira mazuri ya nyuki ili kuhakikisha uchavuaji bora na endelevu kwa nyuki . Hakikisha unaacha mazingira kama ya shamba katika hali ya uasilia.

6. Nyuki hulinda bayoanuai,: uchavuaji ni moja ya mchakato muhimu wa kiasili ambao huchangia katika bayoanuai ya dunia, unatusaidia kuzalisha aina mbalimbali za mimea ambayo asilimia kubwa ni ya chakula. Asilimia 90 ya miti ya maua kote duniani inategemea uchavuaji kwa ajili ya kuzaliana.