Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wanabeba gharama ya vita Sudan kusini , sasa wana fursa ya kuvikomesha:Lacroix

Alice Senna Philip, mwenyekiti wa kikundi cha wanawake jimboni Yei nchini Sudan Kusini akizungumza mbele ya ujumbe wa ngazi ya juu wa UNMISS ulioongozwa na mkuu wao David Shearer. Ujumbe huo ulitembelea eneo hilo.
UNMISS/Francesca Mold
Alice Senna Philip, mwenyekiti wa kikundi cha wanawake jimboni Yei nchini Sudan Kusini akizungumza mbele ya ujumbe wa ngazi ya juu wa UNMISS ulioongozwa na mkuu wao David Shearer. Ujumbe huo ulitembelea eneo hilo.

Wanawake wanabeba gharama ya vita Sudan kusini , sasa wana fursa ya kuvikomesha:Lacroix

Amani na Usalama

Wanawake, wasichana na Watoto nchini Sudan Kusini ndio wanaobeba gharama kubwa ya vita, huku maelfu wakipitia madhila ya kubakwa, utekaji, kunyimwa haki, kutawanywa na hata vifo. Lakini sasa wana fursa kubwa ya kuleta amani. John Kibego na tarifa kamili

Hapa ni katika moja ya makazi ya Umoja wa Mataifa ya ulinzi wa raia mjini Juba nchini Sudan Kusini maisha yakiendelea wakati alipozuru mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean Pierre Lacroix na kuzungumza na wanawake mbalimbali kuhusu mchango na jukumu lao katika utekelezaji wa mkataba wa amani ukizingatia kwamba wao na watoto wao ndio waathirika wakubwa wa vita vilivyoingia mwaka wa sita nchini humo. Miongoni mwao ni Mary Akech Bior kutoka kundi la kina mama wa sudan Kusini

SAUTI YA MARY AKECH

“Hakuna mtu anayesaidia wanawake wa Sudan kusini na tunaiangalia dunia na kujiuliza nini kinachoendelea. Kila wakati watu huja kwetu na kutuuliza wanawake wa Sudan Kusini wanasema nini? Mnafanya nini? Mnaonaje mabo? Lakini hatuna watu wa kutusaidia, kama usambazaji wa makubaliano ya amani , kama nilivyosema itakuwa vyema kwa wanawake wa Sudan Kusini kufanya hivyokwa kushirikiana na asasi za kiraia kwa sababu ndio tulio wengi na ndio waathirika wakubwa wa vita. Hatuna nasaba yoyote na vita na dhamira yetu ni kuwa na amani katika taifa letu.”

Wanawake hao sasa wanasema ni wakati wa hatua kutoka kwa uongozi wa nchi yao na jumuiya ya kimataifa kutekeleza ahaki za amani kwa vitendo. Jean Pierre Lacrois ni mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa

SAUTI YA JEAN PIERRE LACROIX

“ kama hakuna chochote kitakachotokea katika miezi sita ijayo tutasalia katika hali ileile tuliyonayo leo, kwa hakika tunadhani kwamba endapo hakuna chochote kitakachofanyika hali itakuwa mbaya zaidi miezi sita ijayo, hivyo ni muhimu sana kufanya kila tuwezalo. Mnaweza kutegemea AU, IGAD na Umoja wa Mataifa, kwani tumedhamiria kusaidia amani na utekelezaji wa mkataba. “

Makundi ya wanawake nchini Sudan Kusini pia yanataka pande husika kutekeleza ahadi ya asilimia 35 ya wanawake kwenye vikosi vya ulinzi na serikali mpya, kama anavyohimiza mwenyekiti wa muungano wa kitaifa wa Sanu Theresa Cirisio

SAUTI YA THERESA CIRISIO

Wanawake wameteseka sana na vizuri kwamba wanawake wa sudan kusini wana mnepo na wanasonga mbele katika kujaribu kuvishinda vita hivi.”