Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR yaitaka Malta kuangalia upya mashtaka  dhidi ya wahamiaji

Picha ya maktaba katika bahari ya Mediterania, boti ikiwa imewabeba wahamaji na wanaotafuta hifadhi.
UNHCR/L.Boldrini
Picha ya maktaba katika bahari ya Mediterania, boti ikiwa imewabeba wahamaji na wanaotafuta hifadhi.

OHCHR yaitaka Malta kuangalia upya mashtaka  dhidi ya wahamiaji

Wahamiaji na Wakimbizi

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa  OHCHR imetoa wito kwa mamlaka huko Malta kuangalia tena mashtaka yanayohusu ufisadi dhidi  ya vijana watatu waliokamatwa tarehe 28 Machi baada ya kutia nanga nchini humo chombo kwa jina El Hiblu.

Mashtaka hayo yanahusu kisa kilichotokea mwisho  mwisho  mwa mwezi  Machi, wakati wahamiaji 100 waliojaribu kuikimbia Libya waliokolewa katika bahari ya kimataifa na chombo kingine cha biashara kilichokuwa safarini kwenda Libya.

Inaripotiwa  kuwa chombo hicho kiliwaokoa wahamiajiia hao baada ya kuwajulisha kuwa watapelekwa Ulaya lakini  badala yake kikageuka na kuelekea nchini Libya. Wahamiaji hao walipinga vikali kisha chombo hicho tena kikageuka kwenda Malta.

Mashtaka yanayotiliwa shaka

Wanaolaumiwa wana umri wa  miaka 15, 16 na 19, wameshtakiwa chini ya sheria za Malta  kwa kuteka nyara meli na kuilazimisha kueleka Malta. Baadhi ya mashtaka adhabu yake ni kifungo cha maisha. Watatu hao watafikishwa mahakamani Mei 20.

Huku sababu  za uamuzi wa nohodha kugeuza chombo hicho kwenda Malta ukipingwa,  OHCHR imeelezea wasiwasi kuhusu mashtaka hayo. Licha ya kuwa wawili kati yao ni watoto, wote watatu walizuiwa katika gereza lenye ulinzi mkali la watu wazima baada ya kudaiwa jkuhojiwa  na mamlaka bila ya kupewa mshari wa sheria au bila ya kupewa usalama wanaostahili kama watoto.

Ushirikiano katika kutafua na kukoa wahamiaji

“Tumeeleza wasi wasi kwa mamala za Malta kuhusu wanavyotendewa vijana hawa wahamiaji na kile tunaamini kuwa mashtaka yasiyostahili dhidi yao na kuwataka kuyaangalia tena mashtaka hayi, alisema msemaji wa OHCHR Ravina Shamdasani.

Kwa mara nyingine tunataka  Muungano wa Ulaya na nchi wanachama kuwa na ushirikiano unaombatana na haki za bindamu kujibua uhamiaji kutoka Libya.

Nchi zanastahili kuhakikisha  uwepo wa shughulia za kutafuta na kuokoa katika bahari ya Mediteranea.

Nchi ni lazima zihakikishe kuwa wahamiaji waliookolewa wanashuka katika bandari salama ambapo haki zao zitaheshimiwa na kutoa hakikisho kuwa hawatarudishwa moja kwa moja kwenda Libya.”