Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasaka hifadhi 90 wafa maji pwani ya Libya

Wahudumu wa afya wakiwa wamembeba mmoja wa manusura wa tukio la kuzama kwa moja ya vyombo vya majini kwenye bahari ya Mediteranea.
PICHA: UNHCR/F. Malavolta
Wahudumu wa afya wakiwa wamembeba mmoja wa manusura wa tukio la kuzama kwa moja ya vyombo vya majini kwenye bahari ya Mediteranea.

Wasaka hifadhi 90 wafa maji pwani ya Libya

Wahamiaji na Wakimbizi

Taarifa zilizotolewa leo na  Shirika la Umoja wa mataifa la uhamiaji IOM z inasema, wahamiaji 90 wameripotiwa kufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka na kuzama katika bahari mediteranea pwani ya Libya. Patrick Newman na maelezo kamili .

Shirika hilo linasema wahamiaji wanaendelea kupoteza Maisha kila uchao wajaribu kwenda kusaka mustakhbali bora. Kufuatia mkasa huo Bi Olivia Headon ambaye ni mwakilishi wa IOM Libya akizungumza  na wandishi wa habari kwa njia ya simu mjini Genevia  amesema..

(Sauti ya Olivia Headon)

Watu wapatao 90 wamekufa maji wakati boti waliokuwa wakisafiria kupinduka mapema hii leo ,miili ya wa watu 10 kati yao, wawili wakiwa  raia wa Libya na wanane  kutoka Pakistan imeokolea pwani ya Libya, wakati huohuo vikosi wa uokowaji vya Libya vimeripoti kuokoa watu wawili walioweza kuogelea hadi nchi kavu na mmoja kuokolewa na wavuvi bahari.

Kwa mujibu wa ripoti ya IOM ya mwaka jana zaidi ya wananchi 29 wa  Libya waliripotiwa kuokolewa wakijaribu kwenda kusaka hifadhi ughaibuni.

Halikadhalika wasaka hifadhi elfu tatu kutoka Pakistan wameripotiwa kuingia Italia kupitia Libya mwaka 2017, ikilinganishwa na 240 katika  mwezi wa januari 2018 .