Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama na afya kazini ni haki ya kila mtu:ILO

Wanawake katika jimbo la Copperbelt nchini Zam,bia wanaofanya kazi katika mfumo wa kilimo bora wanaongeza uzalishaji wa mbogamboga wanaouza katika masoko ya wenyeji( kutoka maktaba 2015)
ILO/Marcel Crozet
Wanawake katika jimbo la Copperbelt nchini Zam,bia wanaofanya kazi katika mfumo wa kilimo bora wanaongeza uzalishaji wa mbogamboga wanaouza katika masoko ya wenyeji( kutoka maktaba 2015)

Usalama na afya kazini ni haki ya kila mtu:ILO

Ukuaji wa Kiuchumi

Katika kuadhimisha miaka 100 ya shirika la kazi ulimwenguni ILO ambalo dhamira yake ni kuhakikisha ajira bora na zenye hadhi kwa kila mtu, leo ikiwa ni siku ya usalama na afya kazini limetoa wito kwa serikali, waajiri na wafanyakazi kushiriki katika kujenga mazingira salama na yenye afya kazini.

Siku ya usalama na afya kazini duniani yaadhimishwa leo .Siku hii inajaribu kutathimini yaliyopfanywa na ILO katika miaka 100 ya utendaji wake. Ambapo miongoni mwa malengo yake ni kutathimini mafanikio yaliyopatikana katika nyanja ya usalama na afya kazini na kupiga darubini ya siku zijazo hasa kuangalia changamoto kubwa zitakazolikabili soko la ajira kutokana na masuala kama teknolojia , maeneo , maendeleo endelevu SDGs, mabadiliko ya tabianchi na kazi za shirika la ILO.

Utamaduni

Kwa ILO ni lazima kuhakikisha utamaduni wa usalama na afya katika soko la ajira ambapo haki ya usalama na afya katika mazingira ya kazi inaheshimiwa katika ngazi zote. Afisa wa ILO kuhusu masuala ya ajira amesema “Siku ya leo lengo lake kubwa ni kampeni ya kimataifa ya kila mwaka ya kuchagiza usalama , afya na ajira zenye hadhi”

Paneli za sola zitumiazo jua zinatoa nishati safi inayojali mazingira kwa Wazambia wengi (kutoka maktaba)
ILO/Marcel Crozet
Paneli za sola zitumiazo jua zinatoa nishati safi inayojali mazingira kwa Wazambia wengi (kutoka maktaba)

Ameongeza kuwa kwa serikali , waajiri na wafanyakazi ni lazima washiriki katika kujenga mazingira hayo kupitia mfumo unaoainisha bayana haki na wajibu au majukumu.

Mwaka 2003 ILO ilianza kuadhimisha tarehe 28 Aprili kama siku ya usalama na afya kazini ili kusisitiza haja ya kuzia ajali na magonjwa kazini na kuchagiza majadiliano ya kijamii kuhusu suala hilo.

Maadhimisho haya ni sehemu muhimu ya mkakati wa kimataifa wa ILO kuhusu masuala ya afya na usalama ambayo ni moja ya nguzo yake muhimu ya kutetea haki. Siku hii ya kimataifa kwa mujibu wa shirika hilo ni nyenzo muhimu ya kuelimisha umma umuhimu wa afya na usalama kazini.

Wajibu wa serikali

Shirika la ILO linazikumbusha serikali kuwa zinawajibika kwa utekelezaji wa sharia na huduma zinazohitajika kuhakikisha kwamba wafanyakazi wana fursa ya ajira ikiwa ni pamoja na kuunda sera na mifumo ya ufuatiliaji ya kuhakikisha sharia hizo zinafuatwa hasa sera za usalama na afya kazini.

Kwa upande mwingine ILO imetoa wito kwa wafayankazi kuhakikisha kwamba wanafanya kazi kwa usalama na kwa kutowadhuru wengine, kujua haki zao na kushiriki katika utekelezaji wa hatua za kuzuia madahara.