Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na TEF wawapa tuzo waandishi 10 kwa uandishi bora wa habari za watoto nchini Tanzania

John Kabambala ni mmoja wa washindi 10 wa tuzo za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na Jukwaa la wahariri, TEF, kwa waandishi wa habari 10 ambao wameangazia kwa ubora habari zinazowahusu watoto katika mwaka 2018/19.
UN News Kiswahili

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na Jukwaa la wahariri, TEF, wamewatunukia tuzo waandishi wa habari 10 ambao wameangazia kwa ubora habari zinazowahusu watoto katika mwaka 2018/19.

Usia Nkoma Ledama afisa mawasiliano wa UNICEF Tanzania anasema UNICEF na Jukwaa la wahariri walianza kwa kuwapatia mafunzo waandishi wa habari ili kuwanoa na kupanua uelewa mpana katika masuala ya watoto ambapo tangu mwaka 2017 waandishi wa habari 80 wamepatiwa mafunzo maalumu kisha ndipo likaja wazo la kuwatunukia wale ambao kwa ufanisi mkubwa wamejikita katika kuandika na kutengeneza vipindi vinavyolenga kuwapa sauti watoto, “tunafurahi kwamba ushirikiano huu na jukwaa la wahariri, haujaishia tu katika hatua ya kutoa mafunzo bali unakwenda mbele zaidi katika hatua ya kutambua wale wanaopata mafunzo na kuyafanyia kazi lakini pia kutia chachu kwa wengine na wenyewe kuende;eza bidii katika kuhakikisha masuala ya watoto hayaachwi nyuma katika mstakabali mzima wa habari hapa Tanzania. Na hili ni muhimu sana kwani takribani nusu ya watanzania wote ni watoto”

John Kabambala ni mmoja wa washindi 10 wa tuzo za mwaka huu, hapa anaeleza alivyoipokea tuzo hii, “tuzo hii imenipa hamasa kubwa kwasababu furaha ya mwandishi wa habari ni kuona kazi yake inapata mrejesho. Kwa hiyo kwa kupata nafasi ya kuwa miongoni mwa washindi inaonesha kwamba TEF na UNICEF walisikiliza na kuona kazi zangu. Ni hamasa kubwa na furaha kubwa. ”